Kwa kutambua mchango wa Jeshi kwa Taifa. Benki ya NMB imekuwa ikidhamini mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi “CDF Golf Trophy” kwa miaka sita sasa.
Hayo aliyasema Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mpozi katika halfa ya utoaji zawadi kwa washindi wa mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusiana na michezo mingine Afisa huyo alisema NMB wamekuwa wadau wa michezo ya aina mbali mbali hapa nchini, “Kwa upande wa mchezo wa Gofu tumekuwa washirika wa mda mrefu katika klabu hii ya Lugalo kwani ni mwaka wa sita sasa tunayadhamini mashindano haya,” alisema Mponzi.
Katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa Mponzi alisema, Benki ya NMB imegaramia ivifaa na kutoa fedha taslimu kwa manunuzi ya zawadi za washindi.
Kabla ya utoaji zawadi mwasisi wa uwanja wa Lugalo, Jeneral Mstaafu George Waitara aliwataka majenerali wote wajifunze kucheza gofu ili na wao waje wachuane na Majenerali kutoka Malawi watakaokuja kushiriki katika mashindano ya Gofu ya Waitara Trophy mwaka huu. Katika mashindano hayo naodha wa timu ya Gofu Tanzania - Victor Joseph aliweza kuibuka mshindi baada ya kupata grosi 150 na kuwashinda wachezaji wenzake akiwemo Isiack Daudi, George Sembi, Ally Mcharo na chipukizi Richard Masawe.
Upande wa upigaji wa neti Laurent Sangawe kutoka Klabu ya Lugalo aliweza kushinda kwa ushindi wa jumla, baada ya kupiga mikwaju ya neti 131.Klabu ya Lugalo iliendelea kutawala mashindano hayo upande wa dajaja A baada ya Likuli Juma kumshinda Petar Fiwa kwa “countback “baada ya wachezaji wote kupata neti 150.
Naye Erenest Sengeu kutoka klabu ya Lugalo naye aliweza kumshinda Kesy Mwanapala kutoka Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana kwa “countback” baada ya wachezaji hao kupata neti 151. Klabu ya Lugalo iliendelea kutamba katika mashindano hayo baada Chiku Elias kushinda upande wa wanawake kwa kupiga mikwaju ya neti 153, akifuatiwa na mchezaji mwenzake Sara Denis aliyepata neti 155.
Kwa upande wa grosi upande wanawake nafasi hiyo ilichukuliwa na Angel Eaton kutoka klabu ya Lugalo aliyepata grosi 156 na mchezaji huyo pia alishinda kwa upigaji wa mipira mirefu.
Upande wa wanaume nafasi hiyo ilichukuliwa na Isiack Daudi kutoka klabu ya Lugalo, na upigaji wa mipira iliyofika karibu na shimo ilichukuliwa na Neema Olomi kutoka Arusha Gymkhana.
Mashindano hayo ya Gofu ya CDF Trophy 2020 yameshirikisha wachezaji kutoka Mufindi, Zanzibar, Moshi Gymkhana, TPC, Morogoro Gymkhana, Kili Golf, Gymkhana na wenyeji wakiwa Lugalo Gofu club.
No comments:
Post a Comment