Julai 2020 - Miezi michache tu baada ya kurejea kwa michezo mbalimbali mubashara ndani ya DStv, Kampuni ya MultiChoice na The Walt Disney wametangaza kuingia mkataba utakaosababisha kuongezeka kwa chaneli maarufu za michezo ulimwenguni – ESPN hivyo kuifanya DStv kuwa na chaneli nyingi zaidi za michezo mbalimbali hapa duniani. Makubaliano haya yatawezesha chaneli mbili za ESPN kuwa kwenye kisimbuzi cha DStv hivyo wateja wake wataweza kushuhudia michezo mbalimbali inayoonyeshwa kwenye chaneli hizo maarufu kuanzia Julai 29 mwaka huu.
Chaneli za ESPN zinabeba michezo mingi maarufu Marekani kama vile ligi maarufu ya mpira wa kikapu NBAA, ligi ya mpira wa miguu NFL, ligi kuu ya Baseball MLB na nyinginezo. Chaneli hizo pia huonyesha Ligi ya Uingereza EFL, ligi ya Scotland SPFL bila kusahau ligi mbalimbali za Afrika Magharibi.
Wateja wa DStv sasa wataweza kushuhudia tena mubashara michuano ya NBAA kuanzia 31 Julai 2020 kwa kushuhudia mubashara michezo miwili kila siku.
MultiChoice imewaahidi wateja wake kuwa inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa hawatindikiwi na burudani muda wote wawapo na huduma za DStv na kwa makubaliano haya, sasa wateja wake watakuwa na ulingo mpana wa kushuhudia michezo mingi zaidi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Calvo Mawela, amesema “kwakuwa sisi ni nguli wa kutoa burudani kwa wateja wetu kote barani Afrika, wakati wote hatuchelei kuhakikisha kuwa tunaongeza burudani kwa wateja wetu kwa kuwapatia chaneli zaidi zenye burudani za kila pande ya dunia bila kusahau maudhui murua ya hapa nyumbani”
Makamu wa rais muandamizi wa The Walt Disney Company Africa, Christine Service amesema kuwa kuwepo kwa maudhui ya ESPN ndani ya DStv kutaleta hamasa kubwa kwa watazamaji na kwamba wanafurahi sana kuona kuwa sasa wateja wataweza kushuhudia michezo kabambe na nguli wa michezo hiyo kwa umma wa watazamaji kote Afrika.
Mbali na michezo hiyo, pia kupitia ESPN wateja wataweza kupata filamu mpya na motomoto, tamthilia, habari, Makala na maudhui mengine ya kusisimua.
Kwa maelezo zaid tembelea http://africa.espn.com.
No comments:
Post a Comment