Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 22 April 2020

TAASISI YA VODACOM TANZANIA FOUNDATION YAKABIDHI VIFAA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 300 KWA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR ILI KUPAMBANA NA UGONJWA WA COVID-19

Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kulia) akipunga mkono kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi (hayupo pichani) wakati akikabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zilizotolewa na Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation jana ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona visiwani humo, ambapo walifanya makabidhiano kwa njia ya mtandao. Pembeni ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Shaaban Seif Mohammed wanaonekana kwenye Skrini wakiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia wakati Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation walipokabidhi kiasi cha shilingi milioni 300 kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar jana ili kupambana na kudhibiti ongezeko la virusi vya Corona visiwani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika kwa njia ya mtandao.


No comments:

Post a Comment