Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 22 April 2020

DStv YAENDELEA KUWAZAWADIA WATEJA WAKE. YAJA NA KAMPENI KABAMBE YA ‘DStv TUPO NAWE’


Katika kipindi hiki kigumu ambapo watu wengi wanashauriwa kubaki nyumbani, DStv imeamua kuwazawadia wateja wake maudhui mengi zaidi kwa kuwapandisha daraja punde wanapolipia vifurushi vyao.  

Katika kampeni hiyo ijulikanayo kama ‘Tupo Nawe’ ambayo imeanza rasmi Jumatatu April 20, 2020, wateja wote wa DStv wa kifurushi cha Bomba hadi kile cha Compact plus watapata zawadi ya kupandishwa kifurushi cha juu zaidi punde watakapolipia vifurushi vyao kwani ofa hii ni kwa wateja waliolipia na watakaolipia. 

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Jacqueline Woiso amesema hii ni njia mojawapo ya kuwashukuru wateja wote kwa uaminifu wao na kuendelea kutumia DStv. “Nyakati zote tumekuwa tukiangalia namna bora ya kuwahakikishia wateja wetu huduma bora na maudhui bora na mengi na hii ni njia mojawapo ya kuwatunuku wateja wetu. Tungependa wateja wetu kipindi hiki wasikose burudani, habari na elimu na ndiyo sababu tumeongeza maudhui mbalimbali katika vifurushi vyetu” alisema Jacqueline.

Wateja wote wa vifurushi vya Bomba, Family, Compact na Compact Plus watakaolipia vifurushi vyao vya sasa watapandishwa kwenda kifurushi cha juu yake bila gharama ya ziada ili waweze kuburudika zaidi. Wateja wa Bomba sasa wanaweza kuburudika na tamathilia za kimataifa kupitia FOX huku wakiendelea kujifunza vitu vipya kwa kupitia Discovery Family. Wateja wa Family watapata kujionea sinema mbali mbali kupitia M-Net Movies ActionBET na FOX huku watoto wakiburudika kupitia Boomerang. Wateja wa kifurushi cha Compact watapata nafasi ya kujionea maudhui ya kimataifa na hata burudani za nyumbani kupitia 1 Magic, E! Entertainment, Comedy Central na safu ya sinema kupitia M-Net Movies Binge.  Wateja wa DStv Compact Plus watapata kuburudika na sinema na tamthilia za kimataifa kupitia M-Net na M-Net Movies Premier.

Ili kuweza kupata ofa hii kabambe, hakikisha umelipia kifurushi unachotumia kwa sasa nasi tutakupa chajuu yake kisha kaa kwa utulivu na endelea kufurahia burudani kabambe kwani DStv siku zote ‘Tupo nawe’.

Wateja wa DStv wanaweza kutembelea www.dstvafrica.com kwa taarifa zaidi. Ili kuweza kumudu akaunti yako pakua MyDStv leo kwenye simu yako ya mkononi kwa kupitia Appstore au Playstore au wasiliana nasi kupitia WhatsApp namba +255 677 666 111. Pia unaweza kupakua DStvNow ili kuweza kuangalia vipindi vyako kokote uendapo kwa kutumia simu yako.

No comments:

Post a Comment