Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 5 March 2020

WATOA HUDUMA WA FEDHA KUANZA KUSAJILIWA MWEZI HUU, WAMO MAWAKALA WA PESA KWA NJIA YA SIMU YA MKONONI


Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, Kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Bernard Dadi akizungumza kwenye Semina ya Waandishi wa Habari za Uchumi na Fedha inayoendelea jijini Arusha, kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha, na ufafanuzi zaidi kuhusu kusajiliwa kwa Watoa huduma wa Fedha nchini.
Dadi amesema kuwa usajili huo utakuwa ni wa lazima kwa yoyote atakaye husika na utoaji wa huduma wa Fedha,na kwamba usajili huo unatarajiwa kuanza rasmi Mwezi Machi-Aprili 2020 kwa awamu ya kwanza,na awamu ya pili utaanza Mwezi Mei mpaka Juni mwaka huu.

Akifafanua zaidi kuhusu Kanzidata ya kudumu ya watoa huduma wa kifedha (Financial Services Registry) ,Dadi alisema watoa huduma wa Fedha wote wakiwemo mawakala wa Pesa kwa njia ya simu ya mkononi ni lazima wasajiliwe.

“Kila mtoa huduma wa fedha lazima ajisajili, vinginevyo hataweza kuendelea kutoa huduma hiyo kwa vile mfumo hautamtambua.” Alisisitiza.


No comments:

Post a Comment