Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeeleza azma yake ya kuendelea kuhamasisha taasisi za Umma, wawekezaji binafsi pamoja na kuweka jitihada za kuwawekea mfumo wawekezaji wadogo katika mwitikio wa uwekezaji wa dhamana za Serikali ambao una faida hasa katika kuongeza kipato na kutopoteza Fedha inayowekwa.
Akizungumza leo jijini Arusha katika semina inayotolewa kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, Meneja wa Idara ya Masoko na Fedha wa Benki kuu ya Tanzania (BoT), Lameck Kakulu amesema kuwa kuikopesha au kuwekeza kwa serikali kuna faida kwa kuwa kinachowekwa hakipotei.
Amesema kuwa kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia mwezi Juni hadi Desemba 2019 kumekuwa na mwitikio mzuri wa uwekezaji wa dhamana za Serikali ambapo kumekuwa na ongezeko la wawekezaji kwenye minada inayotangazwa kwa zaidi ya asilimia 103 ukilinganisha na kiwango ambacho serikali ilipanga kukopa kwa kipindi cha nusu mwaka.
No comments:
Post a Comment