Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Grooveback Advert_210725

Grooveback Advert_210725

Tuesday, 17 March 2020

VODACOM YATAMBULISHA PEPPER ROBOT KWENYE MAONESHO YA UBUNIFU DODOMA

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu (kushoto) akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Avemaria Semakafu (kulia) na msafara wake kuhusu kazi anazofanya roboti ajulikanaye kwa jina la Pepper ndani ya banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
Mratibu wa mradi wa Instant Schools ulio chini ya Vodacom Tanzania Foundation, Christine Lucas (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Avemaria Semakafu wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu (kulia) akiwapa maelezo baadhi ya wananchi kuhusu kazi anazofanya roboti ajulikanaye kwa jina la Pepper, walipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknilojia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.

No comments:

Post a Comment