Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 12 March 2020

VODACOM YAJA NA TEKNOLOJIA ITAKAYOWAWEZESHA WAKULIMA KUPATA TAARIFA MBALIMBALI ZA KILIMO KUPITIA MTANDAO WAO

Mkurugenzi wa kitengo cha Vodacom Business, Arjun Dhillon (kushoto) akichangia mada kwenye mdahalo wa teknolojia ya kilimo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Ubunifu uliofanyika jijini Dar Es Salaam, ambapo mkulima anaweza kupata taarifa mbalimbali za kilimo kupitia mtandao wa Vodacom. Wengine ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Geofrey Kirenga na Mshauri wa Sera za Kilimo, Prof. David Nyange. 
Mtaalam na Mshauri wa Teknolojia kwa Wateja wakubwa kutoka Vodacom, Goodluck Moshi akielezea namna mfumo maalum wa kidijita M-KULIMA utakavyowawezesha wakulima kupata dondoo za kilimo kutoka mtandao wa Vodacom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi akizungumza kwenye kongamano la wadau wa kilimo kupitia ubunifu wa kiteknolojia kwa mkulima kuweza kupata taarifa za kilimo, ushauri, bei za mazao, pembejeo na taarifa za hali ya hewa kupitia mfumo maalum wa kidijitali M-KULIMA kutoka mtandao wa Vodacom.

Wadau wa kilimo wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali.


Picha ya pamoja mara baada ya kongamamo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof. Kenneth Bengise (katikati) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari Tanzania, Prof. Kenneth Bengise na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi wakipeana mikono mara baada ya kumalizika kwa kongamano la kilimo.

No comments:

Post a Comment