Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 12 March 2020

VODACOM WAPANDA MITI HOSPITALI YA MLOGANZILA JIJINI DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC Wakishiriki zoezi la kupanda miti katika Hospitali ya Muhimbili eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam wakati walipotembelea katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuwapa pole wagonjwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Meneja chapa na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Kijo akipanda mti katika eneo la Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, wakati walipotembelea wagonjwa katika Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2020.
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kushoto) pamoja na muuguzi wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, Christina Mwandaliwa wakishirikiana kupanda mti wakati wafanyakazi wa Vodacom walipotembelea katika Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Muhimbili eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam, Redemptha Matindi (kushoto) akimshuhudia Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akipanda mti wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea katika Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Muhimbili eneo la Mloganzila jijini Dar es Salaam, Redemptha Matindi (kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, walipotembelea katika wodi za wagonjwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2020 (wapili kulia) ni Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald.Pia wafanyakazi hao walipanda miti katika eneo la Hospitali.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, Redemptha Matindi (katikati) akiteta jambo na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa katika Hospitali hiyo na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2020.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC, wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea Wagonjwa na kupanda miti katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2020.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam, Redemptha Matindi (katikati) akimshuhudia Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimjulia hali mmoja wa akina mama aliyelazwa katika Hospitali hiyo wakati wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom walipotembelea wagonjwa na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2020.
Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald, akimjulia hali mmoja wa akina mama aliyalazwa katika Hospitali Mloganzila jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea wagonjwa na kupanda miti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2020.

No comments:

Post a Comment