Tanzania ina akiba kubwa ya gesi asilia na inahitaji maelfu ya mabasi ya jiji kwa mfumo wa BRT ambayo kampuni ya Scania inaweza kuleta. Kampuni ya Scania imekuwa imefanikiwa kuleta magari ya mfumo wa gesi kwa muda mrefu sehemu mbalimbali duniani kama Amerika Kusini,Ulaya, na Australia.
Moja ya faida ya mabasi yanayoendeshwa na mfumo wa gesi asilia (Compressed Natural Gas) ni kwamba mfumo wake wa injini utasaidia kupunguza hewa chafu (Carbon dioxide) kwa asilimia 20 ambapo CO2 inatajwa kuwa ndio chanzo cha joto kali duniani, itapunguza gharama za uendeshaji, gharama kwa abiria na itaisaidia serikali kuongeza mapatoa kupitia uuzaji wa gesi asilia
Akizungumza na wanahabari katika ofisi kuu iliyoko Vingunguti kando na barabara ya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Tanzania, Lars Eklund amesema Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda, hivyo ufanisi unahitajika na kwamba mazingira yasisahaulike.
‘‘Tunaamini ya kwamba Tanzania inahitaji kuwa na teknolojia mpya ili iendane na kasi ya nchi zilizoendelea.Tanzania ni tajiri sana kwa gesi asilia na ni muhimu kutumia nishati hii ya ndani kwa faida ya nchi, nchi itapata faida sana kwani itapunguza kiasi cha mafuta yanayoagizwa nje." na badala yake inaweza kuuza gesi ya ndani kwa waendeshaji wa ndani. Hakuna njia bora na ni ghari sana kujaribu kubadili injini ya dizeli kuwa injini ya gesi’’. Alisema Bwana Lars Eklund.
Kumekuwa na taarifa kupitia vyombo vya habari kutaka kubadili mfumo wa sasa wa magari ya BRT kutoka injini ya dizeli kwenda injisi ya gesi,suala hili halina tija kiufundi na kiuchumi kwasababu injini ya dizeli imeundwa kufanya kazi katika mzunguko wa dizeli wakati injini za gesi na petroli zinaendeshwa kulingana na kanuni ya Otto na ujazo wa kuziba cheche. Kwahiyo ni muhimu sana kuwepo kwa mipango bora ya upanuzi wa miundombinu ya gesi asili ambapo itasaidia wauzaji na waendeshaji kuthubutu kuwekeza katika bidhaa sahihi za gesi asilia zitakazotumiwa barabarani haraka iwezekanavyo. Alisema Bwana Lars Eklund.
Kama sehemu ya kukuza huduma zake nchini, kampuni ya Scania Tanzania inatafuta kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kufadhili wanafunzi wanaochukua elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia (Compressed Natural Gas). Hii itasaidia kuongezeka kwa idadi ya mafundi na wataalamu katika uwanja huo hivyo kuongezeka kwa msaada kwa watumiaji wa mabasi yenye mfumo wa gesi nchini. Mpango huu sio tu sehemu ya kujitolea kuboresha huduma lakini pia ni njia ya kurudisha fadhila kwa jamii zetu zinazotuzunguka. Alisema Bwana Eliavera Timoth,Meneja Masoko Scania Tanzania
KUHUSU SCANIA TANZANIA LIMITED
Kampunia ya Scania Tanzania inafanya kazi kama kampuni ndogo ya Scana CV AB yenye makao makuu yake nchini Sweden. Kampuni ya Scania Tanzania inajihusisha na uingizaji na usambazaji wa bidhaa za Scania nchini. Kampuni hii ina ofisi sehemu mbali mbali nchini ambapo makao makuu yake ni Dar es Salaam, huku ofisi nyingine ni Mwanza,Arusha, na Mbeya.
No comments:
Post a Comment