Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 24 September 2019

DKT. MPANGO AZITAKA BENKI KUFIKISHA HUDUMA VIJIJINI

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), uliofanyika hive karibuni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake, Dkt. Mpango alisema kuwa Tafiti zinaonyesha Kuwa upanuzi wa huduma shirikishi za fedha unaweza kuongeza pato ghafi la taifa kwa kati ya asilimia 10 mpaka 15 kwa mwaka. Kutokana na tafiti hizo, asilimia 28 ya watanzania bado hawajafikiwa kabisa na huduma za kifedha, pia katika asilimin 65 ya waliofikiwa na huduma hizo, ni asilimia 17 tu wanaozipata kupitia mabenki, hivyo kuyataka mabenki kufikisha huduma zake kwenye maeneo ya vijijini na kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), Abdulmajid Nsekela, akizungumza katika Mkutano wa Umoja huo, uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam, ambapo alisema kuwa mabenki yataendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa kuwawezesha watanzania wengi zaidi kupata huduma za kifedha.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kanuni za Mwenendo za Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) pamoja na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) katika Mkutano wa Umoja wa Mabenki, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga na kulia ni Waziri wa Viwanja na Biashara, Innocent Bashungwa.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kushoto) akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) na Makamu wake, Sanjay Rughani, baada ya uzinduzi rasmi wa Kanuni za Mwenendo za Umoja wa Mabenki Tanzania, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanja na Biashara, Innocent Bashungwa na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), Abdulmajid Nsekela, Makamu wake, Sanjay Rughani pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Tusekelege Mwaikasu-Joune, wakikabidhi zawadi ya ngoma maalum kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, baada ya uzinduzi rasmi wa Kanuni za Mwenendo za Umoja wa Mabenki Tanzania, uliofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. 




No comments:

Post a Comment