Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 13 June 2019

MWENYEKITI MPYA WA BODI NA AFISA MKUU WA UFUNDI WA AIRTEL TANZANIA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA AIRTEL JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Airtel Tanzania PLC, Dkt. Omari Nundu (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso leo alipotembelea Makao Makuu ya Airtel Tanzania yaliyopo jijini Dar es Salaam Mtaa wa Morocco. Mwenyekiti huyo ameahidi kushirikiana na uongozi kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inaleta tija kwa watanzania.
Afisa Mkuu mpya wa Ufundi wa Airtel Tanzania, Dkt. Prosper Mafole (katikati) na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Airtel Tanzania PLC, Dkt. Omari Nundu (kulia) wakisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bw. Sunil Colaso walipotembelea Makao Makuu ya Airtel yaliyopo jijini Dar es Salaam Mtaa wa Morocco leo hii. Mkuu huyo wa Ufundi anaendelea na kazi sasa baada ya kuteuliwa na Serikali ili kujiunga na uongozi uliopo wa Airtel kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inatoa huduma bora zaidi na kuipa serikali faida .
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Airtel Tanzania PLC, Dkt. Omari Nundu (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Masoko na Airtel Money, Isack Nchunda (kulia). Wengine pichani ni viongozi wakuu wa vitengo mbalimbali wa Airtel Tanzania.
Afisa Mkuu mpya wa Ufundi wa Airtel Tanzania, Dkt. Prosper Mafole (kulia) na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Airtel Tanzania PLC, Dkt. Omari Nundu (katikati) wakisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Udhibiti wa Airtel, Bi. Beatrice Singano walipotembelea Makao Makuu ya Airtel Tanzania Dar es salaam leo hii mara baada ya kuteuliwa na Serikali kujiunga na uongozi uliopo wa Airtel kuhakikisha kampuni hiyo inayomilikiwa na watanzania kwa asilimia 49% inatoa huduma bora zaidi na kuipa Serikali faida.
Wakwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akifuatiwa na Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Airtel Tanzania PLC, Dkt. Omari Nundu na Afisa Mkuu mpya wa Ufundi, Dkt. Prosper Mafole wakiwa kwenye kikao cha ukaribisho na baadhi ya wakuu wa vitengo mbalimbali wa Airtel Tanzania.

No comments:

Post a Comment