Afisa Biashara Mkuu wa Kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya inayojulikana kama #AppanaChezea Tigo Pesa App. |
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Hussein Sayed akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya inayojulikana kama #AppanaChezea Tigo Pesa App. |
Meneja bidhaa, Tigo Pesa App Ian Ludovick akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya inayojulikana kama #AppanaChezea Tigo Pesa App. |
- Pakua au huisha App yako ya Tigo Pesa bure
- Wateja wanaotumia #AppanaChezea Tigo Pesa App kufurahia faida nyingi ikiwamo kurudishiwa ada ya malipo, Mbs na muda wa maongezi
Kampuni ya simu inayoongoza katika maisha ya kidigitali Tanzania, Tigo, imeanza mwaka 2019 kwa kutangaza uzinduzi wa App ya Tigo pesa katika kampeni inayojulikana kama #AppanaChezeaTigo PesaApp campaign.
Kampeni ya #Appana ChezeaTigo Pesa App inaenda sambamba na filosofia ilinayojikita kwenye uvumbuzi na kumjali mteja kwa kutoa suluhisho za kidijitali zinazoendana na matakwa ya wateja tofauti tofauti hapa nchini.
Kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu, Kampuni ya Tigo imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye mfumo wa malipo ya kidijitali ukilenga kuwapatia wateja huduma za kifedha zinazoendana na dunia ya kisasa. #AppanaChezea Tigo Pesa App campaign ni hatua mpya ya kuboresha uzoefu wa wateja wanaotumia na watakaotumia huduma ya Tigo Pesa. Pamoja na uzoefu huo mpya na wa kipekee, wateja watakaotumia Tigo Pesa App katika kipindi chote cha promosheni watafurahia faida lukuki kama kurudishiwa ada ya kufanya malipo, Mbs pamoja na muda wa maongezi.
“Leo tunayofuraha kuwaletea watumiaji wa simu janja habari njema. Mteja anapopakua au kuhuisha App yake ya Tigo Pesa, atapata dakika za muda wa maongezi na Mbs bure. Pamoja na ofa hii, mteja wa Tigo atakapotuma pesa kwa mteja mwingine wa Tigo atarudishiwa gharama alizotumia kutuma pesa,” alisema Hussein
Kwa mujibu wa Hussein, Tigo Pesa App imetengenezwa kwa kuzingatia usalama wa hali ya juu kwa mteja anapokuwa anafanya miamala yake. Kupitia App hiyo, mteja wa Tigo pia ataweza kufanya malipo kwa zaidi ya taasisi 300 za Serikali ikiwamo Wizara, Mashirika, Mamlaka mbali mbali na watoa huduma za Serikali
Afisa Biashara Mkuu wa Tigo Tarik Boudiaf alisema “Moja kati ya vipau mbele vya Tigo ni kurahisisha maisha ya wateja wake. Kuangalia salio kupitia Tigo Pesa App pia ni rahisi na ni bure. Kununua kifurushi au muda wa maongezi kumerahisishwa zaidi kwa kuwa unachohitajika kufanya ni kufuata hatua tatu rahisi na utakuwa umekamilisha zoezi hilo. Hii ndiyo sababu watu 9 kati ya 10 wanaotumia Tigo Pesa wameridhika na huduma hii na wanawashauri wasiotumia kuitumia,”
Ikiwa rahisi,haraka na yenye ufanisi kwenye matumizi # AppanaChezea Tigo Pesa App campaign inawaletea wateja App bora na rahisi kutumia kuliko App nyingine zinazofanana nayo zilizopo sokoni. Tigo inamshauri kila mteja kuwa sehemu ya safari ya maisha ya kidijitali kwa kutumia huduma za kidijitali za kifedha zinazotolewa na Tigo. Uvumbuzi huu unaendelea kuwawezesha wateja na wafanyabiashara wa Kitanzania kupata huduma za kifedha pamoja kwa njia ya kidijitali na kuyafanya maisha yao yawe rahisi.
No comments:
Post a Comment