Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 8 February 2019

VODACOM TANZANIA YAJIPANGA KUZINDUA HUDUMA YA KUTUNZA PESA KWA VIKUNDI NA VIKOBA


Kampuni ya inayoongoza kwa mafanikio ya kidijitali Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na benki ya Posta Tanzania wanajipanga kuanzisha huduma maalum itakayokuwa maalum kwa ajili kuweka akiba na kutunza pesa itakayojulikana kama ‘Pamoja Group Saving’. Huduma hii mpya itawezesha wajumbe wa kikundi husika kuhifadhi fedha, kupata mikopo na kuwekeza kupitia M-Pesa.

Inakadiriwa kwamba asilimia 16 ya Watanzania (Watu wazima) ambayo ni sawa na watu milioni 4.4 wengi wao wakiwa ni wanawake, wameungana na kuanzisha Zaidi ya vikundi 50,000 vya kuweka na kukopa pesa vijulikanavyo kama Vicoba na vikiwa vimekusanya fedha taslimu zaidi ya Shilingi bilioni 100 za Kitanzania

Kama kiongozi katika soko la mfumo wa pesa za simu, Vodacom M-Pesa, ilizindua na kubuni njia mbali mbali ambazo zinakidhi mahitaji ya soko na kuwavuta wateja wake katika mfumo wa kidigitalli, hivyo huduma ya Vodacom Pamoja Group Savings imelenga katika kufanikisha hili.

“Naamini kwamba kila mmoja wetu anatambua au amejiunga katika SACOSS, Kikoba au upatu. Vodacom inatambua umuhimu wa vikundi hivi katika kuinua vipato vya watu mbali mbali katika jamii, ndio maana tumetengeneza huduma hii ili kuvifanya vikundi hivyo kuwa fanisi zaidi, lakini pia kuwavuta katika huduma za kifedha za kidijitali” alisema Mkurugenzi wa M-Commerce, Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni.

Huduma hii imelenga kutatua matatizo ambayo vikundi hivi vimekuwa vikikumbana nayo kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na usalama, utunzaji wa taarifa, ukusanyaji wa fedha pamoja na ugawaji wa faida ipatikanayo kwa hisa ambazo wamekuwa wakijiuzia ndani ya vikundi hivi. hivyo basi itawawezesha familia, marafiki na vikundi vya upatu kupata huduma za kifedha kwa usalama zaidi na muda muafaka.

Kwa kutumia Pamoja Group Saving washiriki wote wa makundi wataweza kufuatilia mwenendo mzima wa kifedha wa kundi, ikiwemo kiasi cha fedha kilichopo ndani ya kundi. Huduma hii ni ya kipeekee na unaongeza uwazi na kupunguza ugumu na utofauti katika uongozaji wa vikundi, Huduma hii itakuwa kwa wateja wote wa Vodacom pale itakapozinduliwa na itatumika na vikundi vyote vya fedha.

No comments:

Post a Comment