Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 4 February 2019

SPIKA NDUGAI AKUNWA NA UTENDAJI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC), AAGIZA KASI IONGEZWE

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dk Maulidi Banyani (kushoto) hivi karibuni amekutana na Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) na kujadiliana masuala mbalimbali ya maendeleo. Spika Ndugai ameeleza kuridhishwa na kasi ya utekelezaji miradi inayofanywa na Shirika na akahimiza kasi hiyo iongezwe ili kuwapatia Watanzania wengi zaidi huduma ya nyumba hususani wale wa Dodoma yalipo makao makuu ya nchi. 
Spika akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu, Dk Banyani. 
Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk Maulidi Banyani (wa pili kushoto) baada ya mkutano huo.
Spika Ndugai akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.


Wakifurahia jambo baada ya majadiliano ya hoja kadhaa za maendeleo ya sekta ya ujenzi na Shirika kwa ujumla.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk. Maulidi Banyani (wa kwanza kulia) akitoka nje ya jengo la bunge baada ya kukutana na Spika Ndugai. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo na Masoko, Itandula Gambalagi (wa kwanza kushoto) na katikati ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa, Abdallah Migilla.

No comments:

Post a Comment