Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed akikata utepe katika uzinduzi wa tawi jipya la benki ya NIC Tanzania,lililopo katika jengo la Muzammil Centre, Zanzibar. |
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk. Khalid Salum Mohamed akihutubia waageni waalikwa na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la benki ya NIC Tanzania, Zanzibar. |
Tawi hili jipya lililopo kwenye gorofa ya chini ya jengo la Muzammil Centre, barabara ya Mlandege linalenga kuhudumia jamii ya wafanyabiashara wa visiwani, kadiri jamii hio inavyo zidi kukuwa hususan kwenye eneo hilo.
Uzinduzi wa tawi hili unafikisha idadi ya matawi ya NIC kuwa 6 ya kiwemo matawi 5 bara na 1 Zanzibar. Tawi hili litakuwa la kwanza Zanzibar kutoa cheki za kidijitali na huduma ya kuweka fedha benki kutokea maofisini pasina kubidiika kutembelea kwenye tawi. Hii ikiambatana na huduma ya mtandaoni ambayo inawawezesha wafanyabiashara kuangalia miamala wanayofanya kupitia mtandao wa NIC Now.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed aliungana na Wakurugenzi wa Bodi ya Benki ya NIC pamoja na uongozi wa benki hio kwenye uzinduzi.
Katika hutuba yake, Dkt. Salum alisema, “Tunakaribisha uzinduzi wa tawi hili Zanzibar na tunatarajia lita saidia kuboresha uchumi wetu na maisha ya Wazanzibari, lakini pia tunasihi uongozi wa benki hii kutizama namna ya kuisaidia jamii yetu kwenye sekta za elimu na afya.”
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NIC Tanzania, Sharmapal Aggarwal alisema “hili ni eneo linalo kua kibiashara kwa kasi kubwa sana na hii ikiwa ni sambamba na ukuwaji wa utalii. Tunatarajia kupata biashara nyingi huku visiwani na hivyo kuongeza matawi yetu katika miaka ya usoni.”
“Pamoja na miendendo mingine tuliona, kama Benki ya NIC Tanzania, sisi hatutaacha kuendelea na mpango wetu wa utanuzi wa benki letu visiwani. Tuna ari na dhamira ya kukuza mtandao wa benki yetu kwenye maeneo nyeti kiuchumi kote nchi,” aliongezea bwana Aggarwal.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa tawi hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NIC Bi Margaret Karume alisema, “Tuna mkakati madhubuti wa kuongeza matawi yetu kote nchini Zanzibar ikiwemo. Kama benki yenye ubunifu wa kidijitali tunaleta umahiri kwenye usimamizi wa fedha pamoja na huduma za kifedha kwenye simu za mkononi na mtandaoni. Pia, tunawekeza kwenye kufungua matawi mapya kote nchini na huku visiwani ilikuwakaribu na wateja wetu na kuimarisha mtaji wetu.”
“Tunafurahi kuongeza uwepo wetu kwenye mtaa wa kibiashara wa Mlandege na kwa kuzingatia ukuwaji wa biashara na fursa zilizopo pamoja na ushindani mkubwa kwenye sekta ya kibenki, tunatumahi tawi hili litakua kitovu cha biashara na kusaidia ukuzaji wa sekta ya utali Zanzibar.”
“Tawi hili jipya lita beba huduma mbali mbali mahususi kwa ajili ya jamii ya wafanyabiashra kwenye eneo hili. Benki inalenga sketa ya utalii ambayo inakuwa kwa kasi, uwekezaji wa kigeni, uwekezaji wa majengo na mali, pamoja na mashirika na biashara ndogo ndogo,” aliendelea kusema Karume.
No comments:
Post a Comment