Mkurugenzi wa fedha wa DTB Tanzania, Joseph Mabusi (wa tatu kushoto) akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dkt. Amim Kilomoni baiskeli za wagonjwa ambapo pia walikabidhi vifaa tiba mbalimbali ikiwemo ni pamoja na magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa (wa nne kushoto) na wa wafanyakazi wa benki hiyo. |
Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa, akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa DTB Tanzania baada ya wafanyakazi hao kufanya ziara fupi katika hospitali hiyo ambapo pia walikabidhi msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam. |
Kaimu Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Amana, Anna Musa, akitoa maelezo kwa wafanyakazi wa DTB Tanzania baada ya wafanyakazi hao kufanya ziara fupi katika hospitali hiyo ambapo pia walikabidhi msaada wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo;-Baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji vyote vikiwa na jumla ya thamani ya Shilingi 10,000,000/= leo jijini Dar es salaam. |
Mkurugenzi wa fedha DTB Tanzania akizungumza na waandishi wa habari. |
DTB-Tanzania kila mwaka hutenga asilimia 2% ya faida yake kwa ajili ya utekezaji wa shughuli za kijamii. Fedha hizi huelekezwa katika kuboresha huduma katika sekta za Afya, Elimu na Mazingira.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na baiskeli za wagonjwa, magodoro, plasta na vifaa vingine vinavyotumika kwenye upasuaji. Vyote hivi vikiwa na thamani ya Tshs 10,000,000.00.
Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Amana, Dk.Kilomoni alishukuru uongozi wa DTB-Tanzania kwa urafiki uliopo kati ya taasisi hizi mbili ambapo kila mwaka, DTB-Tanzania hutoa msaaada kama huo kwenyeb Hospitali hiyo.
Naye Mkurugenzi wa fedha wa DTB-Tanzania, Ndg. Joseph Mabusi, akiongea na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano alisema, “kama taasisi ya kifedha kamwe hatuwezi kusahau jamii. Ni Dhahiri kwamba faida yetu hupatikana katika kufanya biashara na jamii inayotuzunguka. Kwa mtizamo huo, kila mwaka DTB-Tanzania hutenga fedha ambazo hutumika kwenye shughuli kama hii ya leo”.
Ngd, Mabusi alieleza kwamba DTB-Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo, wamekuwa wakilipa ada ya shule kwa watoto yatima watano kutoka kituo cha Kurasini katika shule ya sekondari ya Sullivan Provost iliyopo Kibaha, pia wamukuwa wakichangia miche ya miti katika Wilaya ya Nyamagana -Mwanza, ikiwa na mtizamo wa kuboresha mazingira katika milima iliyoharibiwa na shuguli za kibinadamu.
DTB-Tanzania kwa sasa ina matawi 28 nchini, 14 kati ya hayo yakiwa jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo (Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco, Magomeni, Mbezi, Mbagala, Nyerere, Kariakoo, Tawi la Nelson Mandela, Upanga lililo barabara ya Umoja wa Mataifa na Tawi la CBD lililo kwenye makutano ya barabara za Samora na Mirambo) jingine ni Tawi Mbezi Chini lililo Kata ya Kawe na tawi jipya kabisa la Mlimani City.
Matawi mengine yakiwemo matawi mawili kwa miji ya Mwanza na Arusha na tawi moja katika miji ya Dodoma, Kahama, Mbeya, Morogoro, Moshi, Mtwara, Mwanza, Tabora, Tanga na visiwa vya Zanzibar.
DTB-Tanzania ni kampuni tanzu ya makampuni ya DTB (DTB Group) yanayoendesha shughuli za kibiashara katika ukanda wa Africa Mashariki nchini Kenya, Uganda na Burundi. DTB Tanzania pia ni kampuni tanzu ya Mfuko wa Aga Khan wa Maendeleo ya Kiuchumi (The Aga Khan Fund for Economic Development – AKFED) ambayo ni tawi la Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network -AKDN).
No comments:
Post a Comment