Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 25 October 2018

UMOJA WA MATAIFA WAZIMISHA MIAKA 73 TANGU KUANZISHWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim akihutubia katika mahadhimisho ya miaka 73 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, katika hotuba yake Mhe. Majaliwa amesema kwamba nchini Tanzania hakuna ubanaji wa uhuru wa vyombo vya habari wala taasisi zisizo za kiserikali.
Aidha, amesema jambo hilo linadhihirishwa na uwepo wa jumla ya vituo vya redio 152, ambavyo kati yake ni vituo vitatu tu ndivyo vinavyomilikiwa na Serikali. Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam 24 Octoba 2018. 
Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ndumbaro, Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodrigues pamoja na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini.
Mhe. Kassim Majaliwa akiagana na Dkt. Ndumbaro mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo. 
Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodrigues naye akiagana kwa furaha na Mhe. Kassim Majaliwa.

Continue Reading

No comments:

Post a Comment