Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan, ameishukuru Benki ya NMB kwa kwa kutoa msaada wa mashuka 108, mashine za kupumulia wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 vikilenga kusaidia kituo cha Maneromango, Kurui na Chole vyote vikiwa wilayani Kisarawe mkoani Pwani. Akipokea vifaa hivyo Makamu wa raisi aliushukuru uongozi wa Benki ya NMB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la afya kwa wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine hapa nchini.
Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Vicky Bishubo alimkabidhi Makamu wa rais Samia Suluhu msaada huo wa vifaa kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokea msada huo mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment