Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday 23 September 2018

ZIARA YA MJUKUU WA MALKIA WA UINGEREZA NCHINI, PRINCE WILLIAM

Prince William.
Mjukuu wa Malkia wa Uingereza “Prince” William anatarajiwa kufanya ziara nchini kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2018. Ziara hiyo inakuja kufuatia maombi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanya naye mazungumzo wakati wa mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uingereza mwezi Aprili 2018.

“Prince” William atakapowasili nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha, atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam; Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.

“Prince” William ni mmoja wa wanaharakati duniani wanaopinga biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori na Uingereza imekuwa ikisifu juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na vitendo vya ujangili.

“Prince” William ataondoka nchini tarehe 29 Septemba 2018 kuelekea nchini Kenya.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 21 Septemba 2018

No comments:

Post a Comment