Mhe. Waziri Mkuu akimkabidhi Bw. Gaunjie kitabu chenye taarifa kuhusu uwekezaji nchini Tanzania. |
Ujumbe wa Tanzania ukifatilia mazungumzo kati ya Waziri Mkuu na Rais wa Kampuni ya Zinjin Gold Mine. |
Mazungumzo yakiendelea. |
Mhe. Majaliwa ambaye yupo nchini China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utakaofanyika tarehe 3 na 4 Septemba, 2018, ametumia fursa hiyo kukutana na Watendaji hao katika hatua za kuhamasisha uwekezaji, biashara na maendeleo nchini.
Katika mkutano wake na Rais wa Kampuni ya NORINCO (China North Indust Bw. Zhang Gaunjie, Mhe. Waziri Mkuu amepongeza uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini hususan kwa kuwa na miradi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania na kuikaribisha kuwekeza zaidi katika maeneo mengine hususan ujenzi wa miundombinu hasa ya Makao Makuu ya nchi. Mhe. Waziri Mkuu alimweleza Rais huyo kuwa, Tanzania inahitaji teknolojia ya kisasa ili kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya makazi hususan kwa Watumishi wa Serikali ambapo sasa Serikali imehamishia Makao Makuu Dodoma.
Kwa upande wake Bw. Zhang Ghaujie alieleza kuwa Kampuni ya NORINCO ambayo imewekeza kwa kiasi kikubwa katika miradi ya Jeshi la Wanachi Tanzania, sasa ipo tayari kushiriki kwenye miradi mingi Zaidi nchini hususan ile ya ujenzi na kwamba kutokana na uwezo na uzoefu mkubwa wa Kampuni hiyo katika sekta ya ujenzi itashirikiana na Tanzania kwenye miradi ya ujenzi wa makao makuu na bomba la mafuta.
“NORENCO ipo tayari kuongeza maeneo ya ushirikiano na Tanzania na inao uwezo wa kushiriki katika kazi za ujenzi hususan kwenye miradi kama bomba la mafuta na Makao Makuu ya nchi” alisema Rais huyo.
No comments:
Post a Comment