Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 4 September 2018

WAZIRI MKUU, MHE. KASSIM MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA BIASHARA KATI YA TANZANIA NA CHINA

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na China ambapo zaidi ya Kampuni 80 kutoka nchi hizi mbili zilishiriki. Wakati wa Kongamano hilo Mhe. Waziri Mkuu alizialika kampuni za biashara na uwekezaji kutoka China kuja kuwekeza Tanzania na kusisitiza kuwa mazingira ya uwekezaji ni mazuri. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini China kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika tarehe 3 na 4 Septemba, 2018 jijini Beijing.
Sehemu ya wageni kutoka Tanzania akiwemo Mzee John Cheyo wakifuatilia mkutano. 
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akitoa neno wakati wa Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. Geofrey Mwambe akiwa pamoja na wageni wengine walioshiriki kongamano hilo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Wang Ke naye alishiriki kongamano hilo. 
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa.
Mhe. Balozi Kairuki akihojiwa na Mwandishi kutoka TBC, Bi. Anna Mwasyoke kuhusu umuhimu wa kongamano hilo kwa Tanzania.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amewakaribisha wafanyabiasha na wawekezaji kutoka China kuja Tanzania kuwekeza kutokana na mazingira rafiki ya uwekezaji na hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.

Waziri Mkuu alitoa rai hiyo wakati akifungua Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na China lililowashirikisha wafanyabiashara zaidi ya 80 kutoka nchi hizi mbili. Mhe. Majaliwa ambaye yupo nchini China kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC) alitumia fursa hiyo kukutana na wafanyabiashara hao ili kuwaeleza hali ya uwekezaji nchini katika

Mhe. Majaliwa alisema kuwa, Tanzania imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuvutia wawekezaji ambazo kwa kiasi kikubwa zimezaa matunda ambapo katika Ripoti ya uwekezaji duniani kwa mwaka 2018 imeitaja Tanzania kuwa kitovu cha uwekezaji kwa ukanda wa Afrika Mashariki ambapo imewekeza takribani dola za marekani bilioni 1.2.

Mhe. Majaliwa aliongeza kuwa, Tanzania inamazingira mazuri sana ya uwekezaji ikiwemo ardhi nzuri kwa kilimo cha mazao mbalimbali kama miwa, mpunga, ngano, mahindi, Mhogo na katani. Alisema kuwa, jumla ya hekta milioni 44 za ardhi zinafaa kwa kilimo na zaidi ya hekta milioni 29 zinafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Akizungumzia sekta ya madini, Mhe. Majaliwa alisema kuwa ni moja ya sekta muhimu inayochangia pato la taifa na kuwahamashisha wawekezaji kuchangamkia sekta hiyo hususan kwenye uchimbaji na uchakataji wa madini ya chuma na uchimbaji wa madini ya urani.


No comments:

Post a Comment