Programu nyingi za mafunzo kwa wahitimu wa vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi duniani kote, zimekuwa zinalenga kuwawezesha wasomi wenye utaalamu katika fani mbalimbali kuwa na dhamira ya kuajiriwa kwenye makampuni mbalimbali yanayohitaji wataalamu. Huwawezesha wahitimu hao kupata msingi na ujuzi kuhusiana na taaluma zao, sambamba na kuwaanda kuwa viongozi wa siku za mbele.
Tofauti na programu nyingine za kuwafundisha wahitimu wa vyuo vikuu kazi, Programu ya Vodacom Tanzania (ambayo imeasisiwa na Vodafone Group) inajulikana kama ‘Gundua Vipaji vya Wahitimu wa Vyuo Vikuu). Humuwezesha mhitimu kufanya kazi kwenye vitengo muhimu vya kampuni.Programu hii ya miaka 2 inalenga kuwapata viongozi wa baadaye wa kuendesha biashara za kampuni kutoka kwa wahitimu wa vyuo vikuu waliobobea katika fani mbalimbali.Kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya hapa nchini, lengo ni kukuza vipaji na kuwapata wataalamu ambao watafanikisha kuiwezesha Vodacom kwenda sambamba na mabadiliko katika sekta ya mawasiliano.
Programu hii ya ‘Gundua vipaji vya wahitimu wa Vyuo vikuu’ nchini Tanzania, ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi Julai, mwaka 2015 na ilianza kwa kupokea maombi ya wahitimu 10 kutoka vyuo mbalimbali ambao walichukuliwa katika awamu ya kwanza ilipoanzishwa.
Ili kujiunga nayo,mhitimu anapitia mchakato mkali uliowekwa, kuhakikisha wanapatikana washiriki wenye sifa zinazostahili. Wahitimu wanafanyiwa tathmini kwa njia ya mtandao, kupitia uelewa wa majukumu watakayotekeleza, tathmini kwa njia ya makundi, uwezo wa kuwasilisha mada na kujieleza na mahojiano ya uso kwa uso. Vilevile, moja ya vigezo vya kuchaguliwa ni kufanyiwa tathmini kuhusiana na ujuzi unaofaa kwa shughuli za kampuni na jinsi anavyoelewa kanuni za kazi za kampuni ya Vodacom (kuhudumia wateja kwa ufasaha, kuwa mbunifu, uwezo wa kutatua changamotoharaka, kuwa tayari kubadilika), mchakato huu una lengo la kuwapata wahitimu walengwa kwenye programu ambao wanafaa na wanaweza kwenda sambamba na utekelezaji wa kanuni za kampuni. Wahitimu wanaofanikiwa kujiunga hupatiwa mafunzo na msaada wanaohitaji ili kuhakikisha kila mmoja anapata ujuzi na uzoefu wa kazi.
Mkurugenzi Rasilimali Watu, Bi. Perece Kirigiti, anakiri kuwa programu imepata mafanikio makubwa tangia kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2015, anazidi kufafanua zaidi mafanikio hayo “Jambo la kipekee na la kufurahisha kuhusiana na programu hii ni mchakato wa kuwapata washiriki wake, wahitimu wanaofanikiwa kushinda na kupata nafasi wanakuwa sawa na wafanyakazi wengine walioajiriwa moja kwa moja na kampuni. Wanaaminiwa kufanya kazi za kila siku za kampuni, wakiwa wanapata maelekezo na mafunzo kutoka kwa viongozi wa vitengo vyao vya kazi,”alisema na kuongeza kuwa wahitimu hao wanapokuwa kwenye mafunzo hayo wanaweza kufanyiwa tathmini kutokana na jinsi wanavyotekeleza kazi zao na kuzungushwa kwenye vitengo mbalimbali ili kuelewa biashara za Vodacom, ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kuwawezesha kufanya kazi wanazopangiwa kwa ufanisi na kuwa wabunifu wa kukabili changamoto mbalimbali.
Sifa nyingine muhimu katika hii programu ni jinsi inavyowezesha wahitimu wanaojiunga nayo kujifunza utendaji kazi kwa haraka kupitia mtandao wa programu unaotekelezwa katika nchi mbalimbali duniani. Baada ya kipindi cha miaka miwili, mhitimu aliyepo kwenye mpango huu anakuwa na sifa ya kuomba kujiunga na programu nyingine ya mafunzo kwa wahitimu ya Vodafone Group, inayojulikana kama Columbus. Wanaofanikiwa kujiunga na programu hii hupata fursa ya kufanya kazi nje ya Tanzania na kuzidi kupata ujuzi na uzoefu kwa ngazi ya kimataifa na kuishia kuwa wafanyakazi wa ngazi za juu ndani ya kampuni.
“Wahitimu wanaojiunga na mpango huu na kufanya vizuri katika kazi za kampuni, wanakuwa na nafasi ya kushindania kupata fursa ya kujiunga na programu ya mafunzo ngazi ya kimataifa ya Columbus, ambayo huwezesha kupata uzoefu wa kufanya kazi mwaka mmoja nje ya nchi, katika kipindi cha muda mfupi tangu kuanza kazi.Tunahakikisha wahitimu hawa wanaendelezwa kwenye fani zao kwa kupatiwa uzoefu wa kazi kwa kuaminiwa na kukabidhiwa majukumu ya kazi siku hadi siku. Ushirikishwa wao huu huwawezesha kuelewa uendeshaji wa biashara za Vodacom vizuri na kuwa na uwezo wa kuonyesha uwezo na vipaji vyao” alifafanua.
Vodacom Tanzania imebaini kuwa programu ya kufundisha wahitimu wasio na uzoefu wa kazi kutoka vyuo vikuu ni njia mojawapo ya kuwapata wafanyakazi wa kuendeleza kazi za kampuni wakiwa wanaelewa misingi ya kazi ya kampuni na ni moja ya njia ya kuwaendeleza wafanyakazi wake kukuza taaluma zao na kuleta mabadiliko katika kipindi kifupi tangia wanapoanza kazi baada ya masomo “Tunao utamaduni tunaojivunia nao wa kuendeleza wafanyakazi wetu. Ni jambo la fahari kwetu kama kampuni kuona vipaji vya vijana wetu vinaendelezwa,” alisema Perece.
Gervas Mfubusa, Keisha Mushi na Amandus Madyane, ni wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao walibahatika kujiunga katika awamu ya kwanza ya Programu ya ‘Gundua vipaji vya wahitimu wa Vyuo Vikuu’ ya Vodacom Tanzania. Walichaguliwa kutokana na uwezo wao na utayari wao wa kufanya kazi na kujifunza kazi kwa vitendo kwa ajili ya kufungua njia za kukuza taaluma zao. Wameweza kutoa ushuhuda wao, wameeleza uzoefu na mafunzo waliyofanikiwa kuyapata kupitia programu hii.
Gervas, ambaye kwa sasa anafanyia kazi katika kitengo cha Raslimali Watu, anasema kuwa Programu hii imemsaidia kwa kiasi kikubwa kupata uzoefu wa kazi “Nilikuwa mwepesi wa kujifunza ili kufanya vizuri katika muda wote nilipokuwa kwenye mafunzo. Nilipata uzoefu mkubwa na kuwa na nafasi ya kuwajibika kufanya maamuzi ambayo yaliweza kuchangia kuongeza mapato ya kampuni,” alisema Gervas.
Kwa upande wa Keisha, anaeleza kuwa mbali na kujifunza kazi alipata bahati ya kufundishwa na wafanyakazi wataalamu na wenye uzoefu mkubwa wa kazi. Alipata fursa ya kufundishwa kazi na Mkurugenzi wa Kitengo alichopangiwa kufanya kazi, alifanikiwa kupati ujuzi mkubwa wa kazi kutoka kwake. ”Tunafundishwa mbinu za kupata ujuzi mpya wa kazi kupitia kupewa majukumu ya kutekeleza kwa kufanya kazi kwa karibu na viongozi waandamizi katika kampuni,” aliongeza kusema Keisha.
Naye Amandus, kwa upande wake aliipongeza programu hii inayowalenga wahitimu kutoka vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi na kuwekeza kwao kwa kuwapatia ujuzi na kuwabadilisha kuwa wataalamu katika kipindi cha muda mfupi.” Kitu mojawapo kikubwa kuhusu Vodacom ni jinsi inavyojikita kuhakikisha mchango wa mshiriki wa programu katika kufanya kazi bila kujali mwonekano wake wa nje-Ingawa ni jambo la muhimu kuwa maridadi kimavazi na kujiamini, lakini mambo hayo sio ya msingi sana wakati wa mchakato wa kuchagua washiriki wa kujiunga na programu hii,” Amandus alifafanua.
Uongozi mzuri na usimamizi ni mambo ya msingi yanayowezesha kupata mafanikio ya Programu ya Kugundua na kukuza vipaji vya wahitimu wa vyuo vikuu wasio na uzoefu wa kazi, wanathibitisha washiriki wake. Wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu wamekuwa wakifanya kazi na kujenga uhusiano wa kikazi wa karibu na wahitimu wa vyuo vikuu wanaokuwa kwenye mafunzo, na kuhakikisha wanawasiliana kwa kila jambo kuhusiana na mambo wanayohitaji kuyafahamu sambamba na kutoa taarifa kuhusiana na majukumu ya kazi wanazokuwa wamepangiwa kufanya.
Gervase, safari yake katika kampuni ya Vodacom imekuwa ni kujifunza kazi na kupata uzoefu “Kufikia matarajio ya mafanikio kunaenda sambamba na kukumbana na changamoto,lakini inafurahisha unapopata mafanikio mazuri kutokana na kutumia vizuri fursa za kukuwezesha kuyafikia”.
“Ukiwa katika programu hii unapata msaada na kutiwa moyo na wafanyakazi wa Vodacom wakati wote, na hii inakufanya ujiamini katika kutimiza majukumu kutumia ujuzi wa taaluma yako”aliongeza Keisha.
Kwa mujibu wa Amandus, Vodacom imekuwa ikitafuta vijana wenye vipaji kwa ajili ya kufanya ubunifu wa kurahisisha huduma wa wateja wake “Maoni na mapendekezo yetu yamekuwa yakisikizwa na kufanyiwa kazi, na hii ili ilitutia moyo kushiriki kuchangia mawazo yetu katika kuboresha kazi na kufanya ubunifu zaidi wa kukabili matatizo mbalimbali yaliyopo katika kuboresha kazi.”
Alipoulizwa anatoa ushauri gani kwa wahitimu watakaojiunga na programu hii katika siku zijazo, Gervas alisema “Wanatakiwa kufanya kazi kwa bidi, wasikilize vizuri wasimamizi wako wanaokufundisha ,kutoogopa kuwauliza maswali unapokumbana na suala ambalo huelewi namna ya kulitatua. Kuwa tayari kukubali kushindwa kwa baadhi ya mambo ila uwe mwepesi wa kujipanga na kuanza tena kujifunza, Hakikisha unazingatia kila unalofundishwa. Kuwa Msikivu na nia ya kujifunza mambo mengi zaidi!”
Keisha, kwa upande wake aliongeza kusema “Siku zote kuwa mstari wa mbele kujifunza, tumia vizuri fursa hii uliyoipata ambayo wapo wenzako wengi hawakufanikiwa kuipata, huwezi amini kwa jinsi utakavyofanya kazi kwa bidii ndio matarajio yako yatakavyotimia.”
Amandus, alisisitiza suala la kuwa myenyekevu unapokuwa katika mchakato wa mafunzo haya, alifafanua zaidi “Programu hii ya kuendeleza wahitimu katika kampuni ya Vodacom ni fursa bora na pekee kuipata, itumie vizuri, kuwa msikivu na kumheshimu kila mmoja. Huwezi kujua nani anaweza kukupendekeza kupata fursa mbalimbali nzuri katika maisha yako.
“Ubora wetu unaletwa na ubora wako” ni kauli mbiu inayotumika Vodacom kuelezea umuhimu wa kuwa na timu nzuri ya wafanyakazi wanaoleta tija na ufanisi katika kampuni inayowafanya waonekane tofauti na wafanyakazi wa taasisi nyinginezo.
Ukifanya kazi Vodacom, unajisikia upo sehemu nzuri kutokana na jinsi kampuni inavyokujali. Afya yako na Usalama mahali pa kazi ni mambo yanayopewa kipaumbele kuliko kitu chochote. Mazingira mazuri ya kazi na taratibu nzuri za kazi ndio yanaifanya Vodacom kuwa Mwajiri Bora nchini Tanzania”, alimalizia kusema Keisha Mushi.
Kampuni imefanikiwa kushinda tuzo ya Mwajiri Bora barani Afrika kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, hii inadhihirisha Vodacom ina mazingira mazuri ya kazi yanayoleta furaha kwa wafanyakazi wake. Ikiwa ni mshindi wa Tuzo za Mwajiri Bora, wenye vipaji wengi wamekuwa wakivutiwa kuajiriwa na Vodacom kutokana na kuwa na mazingira mazuri ya kufanyia kazi ambayo pia yanayavutia vijana wengi wenye taaluma tofauti wanaohitaji kufanya mafunzo ya vitendo.
Wakati kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, ikitambua kuwa kuna mambo mbalimbali katika uendeshaji wa shughuli zake yaliyowezesha kufanikiwa kupata tuzo hii. Programu ya kuendeleza wahitimu imechangia kwa kiasi kikubwa kufikia vigezo vya ushindi huo.
No comments:
Post a Comment