Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 7 September 2018

BENKI YA EXIM TANZANIA YAKAMILISHA KAMPENI YA MIAKA 20 YA KUJALI JAMII

Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Na Watoto, Mh Ummy Mwalimu akikabidhiwa ripoti na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim Tanzania, Jafari Matundu katika kukamilisha kampeni ya miaka 20 ya kuijali jamii. Kampeni hiyo inayoendeshwa na Exim Bank Tanzania imefanikiwa kuboresha huduma za afya kwa kuchangia vitanda na magodoro 500 katika hospitali mbalimbali nchini.
HOTUBA YA NAIBU MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA EXIM TANZANIA JAFARI MATUNDU ILIYOTOLEWA KATIKA KUKAMILISHA KAMPENI YA MIAKA 20 YA KUJALI JAMII SEPTEMBER 4, 2018.
  • MHESHIMIWA WAZIRI WA AFYA,MAENDELEO YA JAMII JINSIA NA WATOTO
  • WAGENI WAALIKWA, MABIBI NA MABWANA.

Kwa niaba ya Menejimenti na wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzanianapenda kuchukua fursa hii Kukushukuru kwa kutupa fursa hii ya kipekee 

Benki ya Exim ni benki ya kiTanzania iliyoanzishwa mwaka wa 1997, na tumetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika nchi za Comorro (2007), Djibouti (2010) na Uganda (2016). Benki ya Exim inafafanua mafanikio kwa jinsi inavyoleta mabadiliko kwa wateja na jamii kwa ujumla na ilitambuliwa kama benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka 2017. Mwaka jana Agosti tulitimiza miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika. 

Benki ya Exim inajivunia kuwa kati ya wadau wakuu wanaosaidia jamii kwenye miradi mbali mbali hasa kwenye sekta ya afya, mazingira na elimu. Benki ya Exim inatambua umuhimu wa jumuiya zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamii ni muhimu sana kwa Benki ya Exim. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa katika kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu. Mifano ya miradi ya kijamii ambayo Benki ya Exim ishajishughulisha nayo ni, misaada ya madawati katika shule tofauti mkoani Morogoro na Babati, miradi ya kutunza mazingira ambapo mwaka jana tulipata tuzo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Ilala, mpango wa damu salama ambao kila mwaka mwezi Juni Benki ya Exim chini ya usimamizi wa Mpango wa Damu Salama wa Taifa hushiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku hii muhimu ulimwenguni kote kwa kufanya kampeni maalum ya kuchangia damu kupitia matawi yake nchini na kuhamasisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii na iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki imewekeza shilling miioni 200 katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake. 

Waheshimiwa wageni tunambua kuna changamoto mbali mbali zinazokabili hospitali za serikali. Katika kukabiliana na changamoto hizi zinazosumbua taifa, benki ya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa iliamuawa kuanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini na mpaka sasa Benki ya Exim imetoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali kumi na mbili katika mikoa 10 nchini kama sehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.

Benki ya Exim inatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii na kwenye ukuaji wa uchumi. Msingi wa mpango wetu huu wa mwaka mzima wa kujali Jamii ni kuelewa kiasi gani wanawake ni muhimu katika jamii. Benki ilijitolea kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 kwa kusaidia wanawake kwa kuboresha huduma za uzazi katika sekta ya afya. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa ya kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu na sisi tumejizatiti kwenye mpango huu. 

Waheshimiwa wageni, Hospitali ya Maweni ya mkoa wa Kigoma ni hospital ya kumi na mbili kupokea mchango huu wa magodoro na vitanda 50, baada ya hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro mwezi Juni ambayo ilipokea vitanda na magodoro 50, hospitali ya serikali ya Sekou Toure ya mkoani Mwanza mwezi Mai ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, hospitali ya rufaa ya Morogoro mwezi Aprili ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, hospitali ya rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam mwezi Machi ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, hospitali  ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mwezi Febuari ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya mwezi Januari ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, hospitali ya Mount Meru, Arusha mwezi Desemba mwaka jana ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba mwaka jana ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba mwaka jana ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba mwaka jana ambayo ilipokea vitanda na magodoro 50 na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana ambayo ilipokea vitanda na magodoro 40.

Benki ya Exim imetoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali za rufaa katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kilimanjaro, Dodoma, Mtwara, Mwanza, Dar es Salaam, Kigoma na Zanzibar. Na itaendelea na mpango wa kujali jamii kwa kutoa misaada mbali mbali katika sekta ya afya. Vitanda na magodoro haya vimesaidia kupunguza changamoto ya wagonjwa kulala chini hasa kwenye wodi za kina mama na mpaka sasa tumewasaidia wagonjwa takribani zaidi ya 300 kwenye wodi hizi katika mikoa mbali mbali. 

Benki ya Exim imekuwa na ushirikiano mzuri na Wizara ya Afya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na tutaendela kushirikiana na serikali katika kuimarisha sekta ya afya Tanzania na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya nchini ili kuboresha taifa.

Asanteni

No comments:

Post a Comment