Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 20 April 2018

VODACOM YAINGIA UBIA WA KIBIASHARA NA KAMPUNI YA IFLIX

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom. Wateja watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom. Wateja watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom. Wateja watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom. Wateja watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Paul Coogan na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan (Kushoto) Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi (katikati) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakiwa kwenye uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom Jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Hisham Hendi (kulia) akikabiziwa zawadi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan (Kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom Jijini Dar es Salaam. Wateja wa Vodacom watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. 
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) akiteta jambo na Meneja Masoko wa Kampuni ya Iflix Afrika Mashariki, Bernice Macharia, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom. Mateja wa mtandao wa Vodacom watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akikabiziwa zawadi na Meneja Masoko wa Kampuni ya Iflix Afrika Mashariki, Bernice Macharia, jijini Dar es Salaam, (wapili kushoto) wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya Iflix na Vodacom. Mateja wa mtandao wa Vodacom watapakua application ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# . Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix Tanzania, Paul Coogan na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Heidi.

Dar Es Salaam, 19 Aprili, 2018 – Kampuni yenye mtandao wa simu za mkononi unaoongoza, Vodacom Tanzania PLC leo imetia saini mkataba wa ubia na kampuni ya iflix, yenye kutoa huduma ya burudani inayoongoza katika nchi zinazoendelea ili kuwapa wateja wa Vodacom huduma hiyo ya iflix bila kikomo. Kampuni hii ya burudani inawapa wateja wa Vodacom uwezo wa kuangalia maelfu ya vipindi bora duniani, sinema na mengine mengi kwenye kila kifaa walicho nacho.

Mteja anatakiwa kupakua App ya iflix, ambapo hakutakuwa na malipo ya aina yeyote. Lakini kuna vifurushi maalum Mteja atabonyeza *149*01# kisha chagua intanet halafu kifurushi ikifuatiwa na iflix. Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 na cha mwezi kwa shilingi 18,000.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kitengo cha Biashara Hashim Hendi alisema: “Vodacom, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini imedhamiria kuiingiza Tanzania katika dunia ya kidijitali na njia mojawapo ya kudhihirisha hili ni kwa dhamira yetu ya kuwapatia wateja burudani isiyo na kifani ya kidijitali. Leo hili linahakikishwa kwa ubia wa kihistoria na kampuni ya iflix. Kuwahakikishia lengo letu la kutoa huduma inayomlenga mteja, siyo tu kuwa tunawapa wateja wetu uwezo wa kufikia burudani bora duniani lakini pia tunajenga jukwaa ambalo wasanii wataweza kutumia kuuza kazi zao. Hii ni hatua kubwa sana kwa Vodacom ikielekea kuwa kampuni ya kidijitali inayoongoza barani Afrika ambayo inawezesha maisha ya kidijitali ya wateja wetu. Tunafurahia sana kuwaleta wateja wetu zaidi ya milioni 12 kwenye huduma za iflix.”

Makubaliano haya yanakuja wakati wa mabadiliko makubwa kwenye vyombo vya habari duniani, mabadiliko yanayoleta ongezeko la uhitaji wa maudhui bora kwenye mifumo mbalimbali. Ikiwa imeshasaini makubaliano na zaidi ya kampuni 240 za usambazaji duniani, iflix inawapa watazamaji wake chaguo kubwa la vipindi vya TV vinavyosifika pamoja na sinema zinazopendwa na mashabiki kitaifa na kimataifa kama vile ICE, Saints I Sinners, Riviera, Britannia, Tin Star, Being Mary Jane, Medici Masters of Florence na Luther, pamoja na nyinginezo. Hii ikiambatana na sinema kubwa za Bollywood kama Love Shagun, Sharafat Gayi Tel Lene, Golmaal Returns and Dedh Ishqiya. 

Muanzilishi wa iflix na Mkurugenzi Mkuu Mark Britt alisema: “Leo ni siku muhimu kwa iflix. Tunafurahi sana kufikisha huduma yetu yenye ubora wa kimataifa nchini Tanzania na kuingia ubia na Vodacom, kampuni ya mawasiliano inayoongoza nchini. Sisi iflix tunashauku kubwa kuwahudumia wateja wa ndani ya nchi ya Tanzania. Tumedhamiria kuwapatia chaguo kubwa kabisa la vipindi vya burudani, kwa uhitaji na matakwa yao wenyewe waweze kutazama au kupakua kwenye kifaa chochote atakachopenda mteja.” 

Upande wa maudhui ya KiAfrika, iflix inatoa sinema za Bongo kama vile Akili Nyingi, Mama Kubwa, Mapenzi Yamerogwa, Family, Perfect Command, Omega na nyingine nyingi huku kukiwa na sinema na vipindi vitakvyokuwa maalum kwa iflix ambavyo vitatangazwa baadae. 

Mkuu wa iflix Afrika Mashariki, Bw. Paul Coogan aliongeza “Tumefurahishwa sana kuileta huduma ya kimataifa ya iflix nchini Tanzania. Ikiwa na vipindi bora kabisa vya TV na sinema kutoka duniani kote, iflix iko tayari kubadilisha kabisa namna ya upatikanaji wa burudani nchini Tanzania. Tunauelewa mkubwa wa watazamaji wa Tanzania na tuna mategemeo mazuri katika ubia wetu na Vodacom kuwafikishia hayo. Huduma yetu nchini Tanzania inawalenga watazamaji wa KiTanzania! Kuanzia uchaguzi wa maudhui hadi jinsi inavyonadiwa, mteja ni kiini wa yote tunayoyafanya.” 

Kwa sasa ikiwa inapatikana katika nchi 27 barani Asia, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini pamoja na barani Afrika kusini mwa Sahara, iflix inawapatia watazamaji maudhui mengi ya sinema kubwa za Hollywood na vipindi vya TV vya kikanda na kitaifa, nyingi kati ya sinema na vipindi vikiwa ni vipya na ndiyo vinarushwa kwa mara ya kwanza. Kila mteja atakapojiandikisha ataweza kuipata huduma hii kwenye vifaa vitano, ikiwa ni pamoja na simu za kiganjani, laptop, tablet na kwenye TV za nyumbani ili aweze kutazama popote na wakati wowote.

No comments:

Post a Comment