Kongamano hilo litashirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na sekta binafsi linatarajiwa kufanyika Februali 23 mwaka huu katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania uliopo jijini Dar es salaam.
Katika tukio hilo, mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama(MB).
Lengo la kufanyika kwa Kongamano hilo ni kujadiliana na makampuni binafsi ya Watanzania kuhusiana na fursa za kibiashara zitakazotolewa kwenye mradi wa bomba la mafuta sambamba na kupeana maarifa ya kupata zabuni ili kuunga mkono maendeleo ya Taifa kwa ujumla wake.
Wakati wa majadiliano kutakuwepo na wawasilisha mada kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC),Wizara ya Nishati na Madini,Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA),Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Mamlaka ya Bima (TIRA) na wawakilishi wa wawekezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta.
Mradi wa Bomba la Mafuta hapa nchini unatarajiwa kufungua fursa mbambali za Kiuchumi kwa makampuni ya Watanzania ambao watanufaika na zabuni zitakazotolewa wakati wa ujenzi wa bomba hilo.
Mapendekezo ya kufanyika kwa kongamano hili yanaangazia ushirikishwaji wa wananchi katika miradi mikubwa ya maendeleo na kuwaonyesha fursa wanazoweza kunufaika nazo.
Washiriki wa Kongamano mnatakiwa kujisajili katika tovuti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi www.uwezeshaji.go.tz au kufika ofisa za Baraza la Uwezeshaji zilizopo Barabara ya Kivukoni jirani na Tume ya Mipango.
Bi. Bengi Issa
KATIBU MTENDAJI,
No comments:
Post a Comment