Habib Kiyombo akikabidhiwa kitita cha Tsh Milioni 1, Tuzo na King’amuzi cha AzamTV kwa kuibuka Mchezaji Bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018. Habib amekabidhiwa zawadi hizo na Afisa Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude na Meneja Fedha wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayella.
Kiyombo amekabidhiwa zawadi hizo dakika chache kabla timu yake haijaingia uwanjani kupambana na timu ya Ruvu Shootings ya mkoani Pwani na anakuwa mchezaji wa pili mzawa kushinda tuzo ya mchezaji bora baada ya Mudathir Yahya kiungo wa Singida United kushinda tuzo ya mchezaji bora katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2017/2018 kwa mwezi Novemba, kabla ya hapo tuzo ilikuwa inachukuliwa na wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania. Mwezi Agosti mshindi alikuwa ni Emmanuel Okwi wa Simba, Septemba akawa ni Shafik Batambuze wa Singida United na mwezi Oktoba akashinda Obrey Chirwa wa Young Africans.
No comments:
Post a Comment