Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 27 January 2018

HALOTEL YAUNGA MKONO JITIHADA ZA KUBORESHA ELIMU TANZANIA

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Pham Dinh Quan (wa tatu kushoto), akikabidhi hundi ya shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu 402 zilizoko jijini hapa katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi Mapinduzi jijini Dar es Salaam. 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Pham Dinh Qual, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi mbalimbali wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu alipokwenda kukabidhi hundi ya shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu 402 zilizoko jijini hapa katika hafla fupi iliyofanyika katika shule ya msingi Mapinduzi jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel Mhina Semwenda, (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari pamoja na viongozi mbalimbali wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu wakati kampuni hiyo ilipo kwenda kukabidhi hundi ya shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, kwaajili ya kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania.
Dar es Salaam - Katika kuunga mkono jitihada za serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa mchango wa fedha taslim Shilingi milioni Hamsini (50,000,000) kwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni moja ya utekelezaji wa kampuni hiyo katika kuunga mkono jitihada za serikali na ofisi hiyo katika kuboresha sekta ya elimu Tanzania, kupitia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402 kati ya hizo shule 295 ni za elimu ya awali/msingi na shule 107 ni za sekondari zilizoko mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi hundi ya mchango huo kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Halotel, Le Van Dai amesema mchango huo ni sehemu tu ya jitihada kubwa zinazofanywa na kampuni hiyo katika kusaidia na kuinua sekta ya elimu nchini ikiwa pia ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuboresha maendeleo ya nchi hasa kupitia sekta ya elimu ambayo ni muhimili wa maendeleo ya kila nchi duniani.

“Tunatambua kuwa, huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na waalimu ni moja ya msingi imara katika kukuza sekta ya elimu nchini, kwa kuzingatia hili tumeamua kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutoa mchango wetu wa kifedha ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa ofisi za waalimu ikiwa ni sambamba na kuboresha mazingira utendaji kazi kwa waalimu ya kazi na kurahishisha ufanisi wao katika kuwafunza wanafunzi ambao ni taifa la leo na kesho” alisema Dai.

“ Halotel tumekuwa mstari wa mbele tukishirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kupitia teknolojia, kwa mfano tumekuwa tukitekeleza mradi wa kuunganisha shule zaidi ya 400 nchi nzima na huduma ya intaneti ni ya kipekee sana, tumeendelea kuhakikisha sisi kama kampuni tunausimamia na kuhakikisha unaleta mabadiliko na tija kwa elimu yetu.” Alisema.

“Katika kuhakikisha mradi huo wa intanenti unawanufaisha waalimu na wanafunzi katika kuboresha uelewa na ufaulu wa masomo yao, Halotel kwa ushirikiano na Ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (CoICT) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) tumeunda jukwaa (Mfumo) wa kujisomea kupitia mtandao wenye masomo ya Sayansi na Hisababati kwa kufuata Mtaala uliokubaliwa na serikali, ambalo unawawezesha waalimu na wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza (I) mpaka cha nne (IV) nchini kote kusoma masomo hayo. Mfumo huu unaoitwa Halostudy, na linapatikana kupitia tovuti

(http://www.halostudy.ac.tz/). Jukwaa hili ni Tofauti na majukwaa mengine yanayofanana, kwa maana maudhui yaliyotengenezwa yameunganishwa na vipengele vya multimedia kama vile video, sauti, na michoro katika maeneo maalum ambapo maudhui mengine ni vigumu kuelewa kutumia maandishi pekee:” Aliongeza Dai.

Kampuni ya simu za mikononi ya Halotel imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali na itaendelea kufanya hivyo katika kuboresha sekta ya mawasiliano nchini, pamoja na sekta nyingine ikiwa ni utekelezaji wa kuboresha maisha ya watanzania kupitia uwekezaji mkubwa uliofanywa na kampuni hiyo nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment