Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakirekodi tuki la uzinduzi wa akaunti mpya ya 'Tukutane Januari' ya Benki ya Mwalimu Commercial Plc jijini Dar es Salaam leo. |
Akizungumzia Kuhusu akaunti hii mpya ya akiba ya ‘Tukutane Januari’, Mkurugenzi Mkuu wa MCB, Bwana Ronald Manongi alisema, mteja ataweza kujiwekea akiba kidogo kidogo wakati wowote katika kipindi chote cha hadi kufikia Januari. Akaunti hii ina riba ya kuvutia ambayo mteja wetu atalipwa kila robo ya mwaka.
Vilevile inamuwezesha mteja wetu kupata mkopo wa hadi asilimia 30 ya amana yake katika kipindi cha mwaka husika. Hivyo Mteja atakapoweka akiba zaidi atafaidika zaidi, na atakuwa na uwezo wa kukopa kiasi kikubwa kulingana na akiba ya akaunti yake.
Akaunti hii ya akiba itamuwezesha mteja kujiondolea usumbufu wa kutatua mahitaji muhimu ya kipesa kipindi cha mwanzo wa mwaka husika ikiwa ni pamoja na ada za shule na vyuo na manunuzi mengine ya vifaa vya shule, pia kodi za nyumba hivyo kuondokana na dhana ya Januari kuwa ni mwezi mgumu.
Mkurugenzi huyo pia aliwaasa watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba mara kwa mara kwani husaidia sana kutatua matatizo mengi yanayoikabili familia na jamii kwa ujumla. “Mara nyingi watu wamejikuta wakiingia katika madeni makubwa na fedheha pale wanaposhindwa kulipa madeni hayo”, alisema Ndugu Manongi. Akiendelea Ndg Manongi alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imebuni mkakati huu kuisaidia jamii kuazimia kupunguza na/ama kuondokana na fedheha, adha na madhara yanayotokana na kuwa na majukumu mazito mwezi huo wa kwanza wa mwaka”.
Naye Mkuu wa kitengo cha Biashara na Masoko aliongeza kwa kusema “Uzinduzi wa huduma hii mwanzoni mwa mwaka 2018 ni moja ya ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Hivyo tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB).
Mlimani Tower - Mezzanine Floor, Sam Nujoma Road
P.O. Box 61002, Dar es Salaam
Telephone: 022-2772954/7 and +255 629 331 151
Email; info@mcb.co.tz
No comments:
Post a Comment