Mudathir alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Beki Asante Kwasi wa Lipuli ya Iringa na Mshambuliaji Danny Usengimana pia wa Singida United, alioingia nao fainali ya kuwania nafasi hiyo. Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa Singida United mwezi huo ikipata pointi saba katika michezo mitatu iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Oktoba hadi ya nne.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa zawadi hizo ikiwemo Dekoda kutoka Azam TV Mudathir amesema “Kikubwa ambacho kimebadilika na kimemfanya niibuke mchezaji bora ni kocha Hans kumwamini kwasababu mtu akikuamini unafanya kile ulichonacho kwa juhuzi zaidi”
Mudathir Yahya anakuwa mchezaji wa kwanza mzawa kushinda tuzo ya mchezaji bora katika Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Tanzania Bara msimu wa 2017/2018. Mwezi Agosti mshindi alikuwa ni Emmanuel Okwi wa Simba, Septemba akawa ni Shafik Batambuze wa Singida United na mwezi Oktoba akashinda Obrey Chirwa wa Young Africans.
No comments:
Post a Comment