Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Hananasifu Idda Uisso akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank baadhi ya mifereji ambayo kwa sasa inatoa maji salama baadhi ya kufanyiwa ukarabati na benki hiyo. |
- Ecobank Tanzania yasaidia kupatikana kwa maji safi kwa Shule ya Hananasif
Msaada huo wa Ecobank Tanzania kusaidia shule hiyo kupata maji safi umetolewa leo ikiwa njia moja wapo ya kuadhimisha kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya Ecobank inayosema ‘Maji Salama, Ishi na Afya njema’ Safe Water, Healthy Living’.
Mbali na Ecobaank kutoa msaada huo, wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pia wamejumuika kwenye kufanya usafi wa mazingira shuleni hapo kwa kuzibua mitaro ya maji taka yote pamoja na kuweka dawa kwenye kisima cha maji shuleni hapo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama.
Kwa upande wa elimu, Ecobank pia imetoa vitabu kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao kuanzia darasa la kwanza hadi la sita.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi Mwanahiba Mzee alisema benki hiyo imekuwa ikiadhimisha siku ya Ecobank kwa kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa Jamii inayowazunguka.
“Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule ya Hananasif ina jumla ya wanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia na sehemu moja tu ambayo inatumiwa na shule nzima. Vyoo havina maji na hivyo imekuwa ni changamoto ya kiafya kwa wanafunzi, walimu na watu wengine kwenye shule hii, tukaona ni vyema kuja kusaidia ” alieleza Mwanahiba Mzee.
Bi Mzee, alisema kutokana na Benki yake kutoa msaada huo, pamoja na vitabu vya kiada, motisha yaa zawadi kwa wanafunzi itasaidia kutoa hamasa kwa wanafunzi kuendelea kuongeza bidii kwenye masomo yao zaidi.
“Ecobank Tanzania inatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora pamoja na kuboresha elimu ikiwa ni dhamira yetu katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu hapa nchini, aliongeza Bi Mwanahiba Mzee.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Hananasif Mwalimu Idda Uisso Alitoa shukrani kwa juhudi za Ecobank Tanzania kwa kuhakikisha shule hiyo inapata maji salama. “Nachukua hii fursa kuwapongeza uongozi wa Ecobank Tanzania kuchagua kuja shule ya Hananasif kwani hapa kuna shule zingine nyingi.
Alisema changamoto kubwa ilikuwa ni maji kwani kwa Idadi kubwa ya wanafunzi walionao maji safi na salama ni muhimu. “Kwa msaada wa mamboresho ya miundombinu yote mliyofanya, kwa sasa tuna uhakika wa maji safi na salama kwa waalimu pamoja na wanafunzi” alisema.
Vile vile alitoa shukrani za dhati kwa msaada wa vitabu pamoja na zawadi kwa wanafunzi bora kwani kutaongeza hamasa kwa wanafunzi. “Sisi kama shule tumekuwa tukifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa lakini kwa msaada wa vitabu na kuhamasisha wanafunzi, nina uhakika na ninawaahidi Ecobank tutaendelea kufanya vizuri zaidi”.
Ecobank sasa inafakisha miaka 8 hapa nchini Tanzania huku ikiwa na matawi ya kutoa huduma bora za kibenki katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha.
No comments:
Post a Comment