Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao mara baada ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC. |
Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo Ijumaa, Mei 5, mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari mbele ya wakuu wa Masoko ya Hisa na Dhamana; Soko la Hisa la Dar es Salaam, viongozi wa Baraza la Uwezeshaji na kampuni ya Vodacom katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amewasihi Watanzania walioko ndani na nje ya nchi wachangamkie fursa ya kununua hisa hizo ili waweze kuwa wamiliki wa kampuni kupitia hisa zao. “Hii ni fursa kwa Watanzania kumiliki kampuni. Ukinunua hisa, unashiriki kikamilifu kumiliki kampuni na pia unaboresha uchumi wako binafsi. Ninawasihi Watanzania wote tumieni fursa hii kununua hisa hizo kabla muda haujaisha ili kuboresha uchumi wetu,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa Vodacom Tanzania itaendelea kuimarisha teknolojia yake ili kuwaunganisha watanzania na kuwezesha kukuza uchumi binafsi. Vodacom Tanzania ilianza kuuza hisa za awali mwezi Machi mwaka huu na mwisho wa kuuza hisa hizo itakuwa ni Mei 11, 2017.
Unaweza kununua hisa kupitia mawakala walioidhinishwa na Mamlaka ya Masoko na Mitaji (CMSA), Benki ya NBC au kupitia M-Pesa kwa kubonyeza *150*36#.
Makundi mbalimbali ya watu wanaendelea kununua hisa za vodacom kwa ajili ya maisha ya baadae. Uuzwaji wa hisa za awali bado unaendelea hadi tarehe 11/05/2017. Waziri Mkuu kaonesha amechangamkia fursa nasi tusibaki nyuma tuwekeze katika uchumi unaokuwa kwa kasi.
No comments:
Post a Comment