Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (Kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) na kupata udhamini kutoka kwa Kampuni ya
mawasiliano ya Zantel akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho mara
baada ya kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuadhimisha hafla
hiyo. Katikati ni Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano
ya Zantel, Kulwa Mbena.
Meneja Mauzo
wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Jensen Msechu(wa pili kulia) akifafanua
kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dar es salaam wakati wa hafla ya
“Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Zantel. Hafla hiyo ilifanyika siku ya
jumamosi katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo. Kulia ni Mkufunzi Mkuu
na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena.
Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwaongoza wanafunzi na baadhi ya wakufunzi
wa chuo kikuu cha Dar es salaam kucheza nyimbo ya “Strength of a woman” ya
Mwanamuziki Shaggy ambayo ina maudhui ya kuwainua wanawake wakati wa hafla ya
“Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla
hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
Baadhi ya
wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Zanaki wakifuatilia hafla ya “Mwanamke
na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es
salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo
ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
No comments:
Post a Comment