Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday, 14 January 2017

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI MKOANI SHINYANGA JANUARI 13, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited cha Mkoani Shinyanga. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck wakwanza kulia mwenye kilemba, mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele wakwanza kushoto, pamoja na mmiliki wa kiwanda hicho Fred Shoo watano kutoka kushoto.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kwenye jiwe la ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited cha Mkoani Shinyanga. Kulia ni mmiliki wa Kiwanda hicho Fred Shoo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mmiliki wa kiwanda hicho cha Fresho, Fred Shoo kuhusu malighafi ya kutengenezea mifuko ya Sandarusi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya hatua za mwisho katika utengenezaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia na kukagua utendaji kazi wa maabara ya kiwanda hicho cha kutengeneza mifuko ya Sandarausi mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda hicho cha Kutengeneza mifuko ya Sandarusi mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Salum Hamis Mbuzi mmiliki wa Kiwanda cha kutengeneza Vinywaji cha Jambo food product mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga Januari 13, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagawia vinywaji kwa wananchi na kikundi cha ngoma za asili cha mkoani Shinyanga mara baada ya kuzindua kiwanda hicho cha Vinywaji mkoani Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product Salum Hamis Mbuzi mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia kwa kuwapungia mkono wakazi wa Igunga mkaoni Tabora.
Ikulu Blog

No comments:

Post a Comment