Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kwanza Mtanzania wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bwana Maharage Ally Chande. |
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya Habari imeeleza kuwa, Mwenyekiti wa MultiChoice Tanzania, Bw. Ami Mpungwe, akiidhinisha uteuzi huo wa Bwana Maharage Ally Chande kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MultiChoice Tanzania, amesema, “MultiChoice Tanzania inaona fahari kuhusu uteuzi huu- hakuna shaka kwamba Bw. Chande ni miongoni mwa watanzania watendaji bora kabisa na anakuja pamoja na uzoefu mkubwa katika masuala ya usimamizi wa taasisi. Sifa zake kama mtaalamu wa huduma za kibenki na kifedha pamoja na tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ni ujuzi tunaouhitaji katika biashara yetu ili kuipeleka biashara ya Tanzania katika viwango vipya vya hali ya juu.
Tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya na bila shaka atawahudumia wateja wetu wa DStv kwa nguvu na juhudi mpya.” Alieleza Mwenyekiti huyo wa Multichoice Tanzania.
Taaluma yake:
Bw. Chande ni mtanzania wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu MultiChoice Tanzania na anajiunga na familia ya MultiChoice baada ya hapo awali kushika wadhifa wa Mkurugenzi Wa Huduma Za Taasisi katika Ofisi Ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (President’s Delivery Bureau).
Pia Bwana Chande amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiutendaji kama Afisa Mtendaji Mkuu katika Benki Ya Taifa ya Biashara (National Bank of Commerce) kampuni tanzu ya Barclays/ABSA-na pia kutekeleza majukumu ya Meneja Mtendaji wa Tekinolojia na Mawasiliano, Data na Huduma za Ongezeko la Thamani.
Ana shahada ya Sayansi katika Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu Cha Afrika Kusini.
Mo Dewji Blog
Congrtulations Mr. Chande, You deserve the appointment, We have no doubt you will prove they were right to put their trust on you! Work smart!
ReplyDeleteCongratulation Maharage Chande Kwa nafasi hiyo najua uwezo wako tangu tukiwa darasani. Unaweza na utafikia matarajio ya kampuni yako Mpya.
ReplyDeleteOngela sana Mungu akutangulie katika majukumu yako mapya ISHAALAH Mungu atatia wepisi kati kazi zako.
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDelete