Shirika la ndege la Etihad ambalo ndio shirika rasmi la nchi ya Falme za kiarabu, leo hii imefungua milango ya kituo cha afya chenye hadhi ya kimataifa kwa ajili ya wafanyakazi wake Abu Dhabi. Kituo hiki ambacho ni kikubwa kwa mazingira kitatoa huduma za kliniki, huduma za kitabibu kwa wafanyakazi wenye visa pamoja na raia wenye vitambulisho toka falme za kiarabu.
Kituo hicho kilichopo jengo la Etihad Plaza, mjini Khalifa, kitaruhusu wafanyakazi zaidi ya 23,800 wa shirika hili la ndege wenye makazi nchi ya Falme za kiarabu kupata huduma bora za kitabibu, katika mazingira ya kisasa karibu kabisa na makao makuu ya shirika hilo la ndege.
Afisa mkuu wa rasilimali watu na Utendaji, Ray Gammell, alisema “Kama muajiri bora zaidi duniani, tunajivunia kwa kutoa huduma kwa timu yetu kubwa ya wafanyakazi, wakiwemo wa nchi ya falme za kiarabu na wakigeni. Kituo hiki kipya kitaruhusu tuendelee kuboresha programu zetu zinazolenga kutunza afya za wafanyakazi wetu na hivyo kuongeza ufanisi wao wa kazi
Upanuzi wa Kliniki mpya ya anga ni sehemu ya mkakati maalumu wa shirika la ndege la Etihad kuwa na kituo cha afya kinachoongoza katika kanda hiyo. Kituo kikiwa na wahudumu wa afya zaidi ya 30 waliobobea, wakiwemo madaktari bingwa 10, vyumba sita vya uchunguzi, vyumba tisa vya madaktari na vifaa vya kisasa kabisa kusaidia wafanyakazi, kliniki ina ahidi kutoa huduma bora kabisa ya kitatibu na afya kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad.
Dk. Nadia Bastaki, makamu raisi wa huduma za afya, alisema “Kliniki mpya yenye viwango vya kisasa kabisa inaonyesha dhamira yetu kuendelea kutoa huduma za afya zenye viwango vya juu kabisa kwa ajili ya wafanyakazi wetu ikiwemo marubani na wahudumu wa ndani ya ndege. Kliniki hii inasimamiwa na mamlaka ya afya ya Abu Dhabi (HAAD) na mamlaka ya usafiri wa anga UAE (GCAA), tukiwa na furaha ya kutambulika kama moja ya kituo kinachoongoza katika huduma za utabibu na vifaa katika sekta ya anga.”
Wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad pamoja na wategemezi wao pia wataweza kupata huduma kutoka kituo hiki cha matibabu ili kusaidia mchakato wa maombi ya VISA. Kuna makubaliano yaliyosainiwa mwezi Februari 2015 na Ambulatory Healthcare Services – SEHA kuendesha kituo hicho na kutoa huduma za vipimo kwa ajiliya Visa kama X-Ray, vipimo vya damu na vipimo vya mwili
Dk. Mariam Buti Al Mazrouei, Kaimu mtendaji mkuu wa Ambulatory Healthcare Services (AHS), alisema: “lengo letu kuu baina ya SEHA na AHS ni kuboresha upatikanaji wa huduma za kiafya na ufunguzi wa kituo cha vipimo kwa ajili ya mchakato wa VISA ni mfano wa jinsi gani lengo letu linaweza kufikiwa kupitia ushirikiano wa wadau kutoka sekta mbalimbali nchini. Kituo kipya kinaleta idadi ya vituo vinavyoendeshwa na AHS kufikia jumla ya vituo kumi na moja, na hivyo kuimarisha nafasi yetu kama vinara wakutoa huduma ya vipimo vya afya kwa ajili ya mchakato wa VISA kwa nchi ya Falme za kiarabu”
Aidha kituo cha mamlaka ya vitambulisho cha Emirate pia kikiwa kimejengwa eneo husika ili kutoa huduma kwa wafanyakazi takribani 200 kupata vitambulisho kila siku. Eneo husika litasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano na mchakato mzima wa kupata vitambulisho vya Emirates kwa wafanyakazi na wategemezi wao hapa nchi ya Falme za kiarabu
Hapo mbeleni kutakuwa na nafasi kwa raia wa Emirate kupata mafunzo na ujuzi wa unesi kupitia mpango wa chuo cha mafunzo ya unesi cha Fatima, kikilenga kuvutia manesi nchini humo kupata ajira katika sekta ya anga pia.
Kituo kipya kinafuatia utambulisho wa huduma ya ambulance kwa wafanyakazi, kliniki maalumu kwa wanaosafiri kikazi, vituo kadhaa vya afya na mazoezi huko Abu Dhabi pamoja na kituo mahususi kwa ajili ya kusaidia ustawi wa marubani pamoja na wahudumu wa ndani ya ndege.
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
No comments:
Post a Comment