Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 18 August 2015

WAZIRI MEMBE ATEMBELEA MABANDA YA MAONYESHO WAKATI WA KONGAMANO LA DIASPORA

Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko, Tuntufye Mwambusi akimpa maelezo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard K. Membe (Mb.) kwenye banda la maonyesho la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo nje ya kongamano la Diaspora la Ubia SMEs 2015 Serena Hotel lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Benard K. Membe (Mb.) akifuatilia maelezo kutoka kwa maafisa wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika banda la maonyesho la Shirika kwenye kongamano la Diaspora la Ubia SMEs 2015 Serena Hotel lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akipata maelezo kuhusu matumizi ya Gesi Asilia, Miradi na manufaa yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. James Mataragio (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa Kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora).
Waziri Membe akionyeshwa na Bw. Mataragio eneo bomba la gesi asilia lilipopita kwenye Mchoro wa Ramani ya Tanzania uliopo mbele yao.


Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika picha ya pamoja na Bibi Dorcas Membe (kushoto), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Mataragio (Kulia), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) na Watumishi kutoka katika shirika hilo.
Waziri Membe na Mkewe Mama Dorcas wakipata maelezo juu ya matumizi ya radio calls kutoka kwa Bw. Sunji wa Kampuni ya Huawei nchini alipotembelea banda la Kampuni ya hiyo wakati wa Kongamano la Diaspora.
Waziri Membe (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) nchini, Bi. Matilda Nyallu. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Balozi Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Balozi Mulamula (katikati) akielezea jambo kwa Waziri Membe (kushoto).
Waziri Membe akisalimiana na mmoja wa Washiriki wa Kongamano la Pili la Diaspora,Bw. William Malecela. Kulia ni Balozi Mulamula na katikati ni Bi. Suzani Mzee kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rosemary Jairo (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa pili kutoka kushoto) na Maafisa Mambo ya Nje Bw. Batholomeo Jungu (kulia) na Bw. Amosi Tengu (kushoto).

No comments:

Post a Comment