Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanzania wanaoishi India katika Hotel ya Taj Palace jijini Delhi. Rais Kikwete aliwaeleza mambo ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile barabara, maji, umeme na uboreshaji wa bandari ya Dar es Salaam. Aidha, aliwaambia mipango iliyopo ya kujenga bandari ya Bagamoyo na reli ya kati ya kisasa. Aliwaeleza pia hali ya kisiasa, hususan maandalizi ya uchaguzi mkuu ambapo zoezi la kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Rais linaendelea. |
No comments:
Post a Comment