Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday, 16 June 2015

BILIONEA ALIKO DANGOTE ALIDHIA UJENZI WA BANDARI YAKE MTWARA KWA KUSHIRIKIANA NA TPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia alipowasili kwenye uwanja wa Ndege mjini Mtwara kwa ajili ya kutembelea kiwanda chake cha saruji kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha saruji cha Dangote. Katikati ni Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Ishaya Manjanbu.

Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kulia), akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, walipokutana mjini Mtwara kuangalia uwezekano wa kujenga kituo cha kusafirisha saruji katika eneo la Bandari ya Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na waandishi wa habari baada kuwasili mjini Mtwara na kutembelea kiwanda chake cha saruji, kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akisaini kitabu cha wageni, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Mtwara, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake cha saruji. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akifuatana na wenyeji wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia (wa pili kushoto), Balozi wa Nigeria, Ishaya Manjanbu (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bi. Fatma Salum Ali (kushoto), alipowasili kwenye uwanja wa ndege, mjini Mtwara.




Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote, akiteta jambo na Mwakilishi mkazi wa Dangote nchini Tanzania, Bi. Esther, mjini Mtwara, baada ya Mkurugenzi huyo kutembelea kiwanda chake cha saruji kinachojengwa mkoni Mtwara.

No comments:

Post a Comment