Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 17 April 2015

MFUMO MPYA WA UONDOSHAJI MIZIGO (TANCIS) KUONGEZA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

Kamishna wa Forodha na Ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Masamaki Kabisi akiwaeleza waandishi wa Habari juu ya faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo bandarini (TANCIS) ikiwa unasaidia katika kufanya makadirio ya kodi sahihi kulingana na taarifa sahihi zilizoletwa kwa kutumia mfumo huo, pia utasaidia wateja kujua sehemu mizigo yao ilipo na pia wanapaswa kulipa kiasi gani kulingana na mzigo wa mteja, wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwandamizi wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Felix Tinkasimile akiwaeleza waandishi wa habari namna mfumo mpya wa uondoshaji mizingo unavyoongeza uwazi na uwajibikaji utakaosaidia kuzuia upoteaji wa mizigo bandarini ikiwemo Magari na Makontena, wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Huduma cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Kasty Phelician akiwaeleza waandishi wa Habari majukumu ya kituo hicho ikiwemo kutoa tathmini ya kodi unayopaswa kulipwa kwa kupitia na kuhakiki nyaraka zote kutoka kwenye kadhia zinazotumia mfumo wa TANCIS ikiwamo viwango vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kutozwa.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakimsikiliza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.Burton Kaissy wakati wa Ziara iliyofanyika katika mamlaka hiyo kuona jinsi mfumo wa TANCIS unavyofanya kazi. (PICHA NA HASSAN SILAYO - MAELEZO).

No comments:

Post a Comment