Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 17 April 2015

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI JIJINI DAR

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkaribisha Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es salaam na kufanya mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China katika masuala ya uendelezaji wa Ardhi na Mipango miji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kulia) akimweleza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (kushoto) namna Wizara yake inavyoendelea kuimarisha shughuli za Mipango Miji, Usimamizi na Matumizi endelevu ya Ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Alphayo Kidata (kushoto) akifurahia jambo wakati akizungumza na ugeni kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania ulioitembelea Wizara hiyo jana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuendeleza ushirikiano kati ya China na Tanzania katika Matumizi endelevu ya Ardhi.
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akitoa ufafanuzi kuhusu uendelezaji wa ushirikiano kati ya China na Tanzania katika katika sekta ya ardhi hususan utoaji wa mafunzo kwa watalaam wa Ardhi, Matumizi endelevu ya Ardhi na Mipango miji nchini. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO).

No comments:

Post a Comment