Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 7 March 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA STUDIO ZA AZAM MEDIA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi studio za kisasa za Azam Media jijini Dar es Salaam jana. Rais Kikwete alizindua studio hizo ambazo ni za kisasa zaidi zilizowahi kufunguliwa katika nchi za Afrika Mashariki na Jangwa la Sahara zilizogharimu sh Bilioni 53. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya Bakhresa, Said Salim Bakhresa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akilakiwa na Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando alipokwenda kuzindua rasmi studio za Azam Media jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa studio za Azam Media jijini Dar es Salaam jana.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Azam Media jijini Dar es Salaam jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, uongozi wa Azam Media pamoja na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya magari ya kurushia matangazo ya moja kwa moja baada ya uzinduzi rasmi wa studio za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Barnaba (kushoto) na Mwansiti Alimasi wakiimba wakati wa hafla ya uzinduzi wa studio za Azam Media jijini Dar es Salaam jana. (Picha na Peter Mgongo).

Bofya hapa kuona picha zaidi

No comments:

Post a Comment