Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 17 March 2015

BENKI YA NMB YAUNGANISHA WAFANYABIASHARA WAKUBWA MKOANI MBEYA

Katika mwendelezo wa kuwa karibu na wateja wake benki ya NMB imezindua mtandao utakaowaunganisha wateja wake wakubwa ‘Executive Network’ kwa jiji la mbeya ikiwa na lengo la kuwafanya kufurahia zaidi huduma za kibenki kutoka NMB.

Uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Mbeya na kuwakutanisha wafanyabiashara zaidi ya 100 kutoka vitongoji mbali mbali ikiwemo Kyela, Mbozi, unduma, Mwanjelwa, Mbalizi Road na Usongwe waliopata fursa ya kuwa kwenye mtandao wa wafanya bishara wa NMB.

Mtandao huu unaounganisha wateja wakubwa wa NMB vile vile umezinduliwa katika mikoa mbalimbali ikiwemo; Arusha, Mwanza, Dar es Salaam na Mbeya ikiwa ya nne.

Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa NMB, Richard Makungwa (pili kulia) pamoja na Given Ngajilo wa kampuni ya Tunhimbaghe Traders Ltd (mteja), wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB Executive Network jijini mbeya huku wakishuhudia ni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa NMB, Filbert Mponzi (kulia) na meneja wa NMB Nyanda za juu, Lucrecia Mkarie.
Maafisa wa NMB wakifurahi pamoja na mteja wao baada ya uzinduzi rasmi wa mtandao wa ‘NMB Executive Network’.
Sehemu ya wateja wakubwa wa NMB walioalikwa katika uzinduzi huo.
Mmoja wa wateja wakubwa wa NMB akiomba ufafanuzi juu ya huduma zitolewazo na benki hiyo wakati wa hafla iliyowakutanisha wateja wakubwa wa benki ya NMB.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa NMB, Masato Wasira (kushoto) na Mtaalam Mwandamizi wa bidhaa za hazina kwa wateja wakubwa, Ronald Kato wakiwa pamoja na wateja wa NMB kutoka kampuni ya Sunshine Mining ya Chunya.

No comments:

Post a Comment