Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 16 February 2015

BENKI YA NMB YAANZA KUTOA HUDUMA KUPITIA MAXMALIPO KWA MAFANIKIO

Mkazi wa kigamboni akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa NMB jinsi anavyoweza kupata huduma ya kibenki kutoka kwa wakala wa NMB kwa kupitia kwa mawakala wa Max malipo na huduma ya NMB Wakala.
Wasanii wakiwatumbuizia wananchi wa Kigamboni katika tamasha la kuelimisha matumizi ya huduma ya NMB Wakala.
Ofisa wa NMB akitoa maelezo ya namna ya kupata huduma za NMB kwa kutumia mashine ya MaxMalipo.
BENKI ya NMB imeanza kutoa huduma zake kupitia mawakala wa MaxMalipo kwa mafanikio katika hatua ya majaribio inayoendelea Kigamboni – Dar es Salaam, Dodoma na Arusha.

Huduma hiyo inayojulikana kama NMB Wakala itakuwa inapatikana kwenye maduka ya kawaida yenye huduma za MaxMalipo, inategemewa kusogeza huduma za benki hiyo mpaka vijijini na kuwa benki ya kwanza kuweza kupenya maeneo ya vijijini.

Kwa ajili ya kuhakikisha huduma hii inawafikia wengi, NMB inafanya matangazo katika eneo la kigamboni kuhamasisha wakazi wa eneo hilo wanapata elimu zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya NMB wakala. Katika promosheni hii mwananchi yeyeote anaweza kufungua akaunti na kupata Kadi ya ATM papo hapo.

Kwa sasa NMB imemaliza kufanya majaribio katika eneo la Kigamboni – Dar es Salaam kwa mafanikio makubwa na hivyo kuwa tayari kuanza kutoa huduma hiyo nchi nzima huku malengo ya awali ikiwa kuwa na mawakala Zaidi ya 3,000 nchi nzima.

No comments:

Post a Comment