Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 16 February 2015

BENKI YA NBC NA ENVIROCARE KUWAKOMBOA VIJANA KUPITIA MRADI WA MAZINGIRA

Naibu Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Catherine Jerome na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia) wakionyesha kipande cha mkaa uliotengenezwa na taka za karatasi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati wakizungumzia kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika mtaa wa ubungo kibangu na jinsi takataka zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi. Kampeni hiyo imefadhiliwa na benki ya NBC.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Catherine Jerome (kushoto) akionyesha kipande cha mkaa uliotengenezwa na taka za karatasi jijini Dar es Salaam jana, wakati wakizungumzia kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika mtaa wa ubungo kibangu na jinsi takataka zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi. Kampeni hiyo imefadhiliwa na benki ya NBC. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa.
Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (kulia), akizungumza kuhusu ufadhili wao kwa asasi isiyo ya kiserikali ya Envirocare jijini Dar es Salaam mwishoni jana, kwa kampeni yao ya kuhamasisha utunzaji mazingira katika mtaa wa ubungo kibangu na jinsi takataka hizo zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri.
Ofisa Miradi wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Israel Richard (kushoto), akimwonyesha Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Rukia Mtingwa (wa tatu kulia) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, mashimo ya kutengenezea mbolea kutokana na takataka ikiwa ni sehemu ya kampeni yao ya kuhamasisha utunzaji mazingira na jinsi takataka hizo zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali. Wa pili kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter, Naibu Mkurugenzi wa Envirocare, Catherine Jerome na Meneja Rasilimali Watu wa asasi hiyo, Carolyn Mwanry (kulia).
Meneja Rasilimali Watu wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Carolyn Mwanry (wa pili kulia) akishiriki kufanya usafi na baadhi ya wakazi wa mtaa wa ubungo kibangu, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira na jinsi takataka hizo pia zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri. Kampeni hiyo imefanyika chini ya ufadhili wa benki ya NBC.
Meneja Rasilimali Watu wa Shirika lisilo la kiserikali la Envirocare, Carolyn Mwanry (kulia), Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa kibangu, Desdery Ishengoma (kushoto) na Diwani wa kata ya makuburi, William Mwangwa wakishiriki kufanya usafi na baadhi ya wakazi wa mtaa wa ubungo kibangu, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhamasisha utunzaji mazingira na jinsi takataka hizo pia zinavyoweza kuleta fursa za kiuchumi na kusaidia vijana kujiajiri. Kampeni hiyo inafanyika chini ya ufadhili wa benki ya NBC. (Picha zote na Peter Mgongo).

No comments:

Post a Comment