Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 21 January 2015

NHC YAENDESHA KONGAMANO LA MAMENEJA WA MIKOA NA WATENDAJI WAKE KATIKA HOTELI YA NAURA SPRINGS, ARUSHA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza jambo katika kongamano hilo ambapo alisisitiza umuhimu wa Watendaji wa NHC kuongeza ubunifu katika kazi zao ili kuongeza ufanisi wa kazi zao.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akikabidhi zawadi ya simu ya kisasa ya I Phone 6 kwaajili ya kuboresha ufanisi kwa Ofisa Mwandamizi Uendelezaji Biashara Fatima Rajabu ambaye aliibuka mshindi wa jumla wa maigizo ya vitendo kwenye kongamano la Mameneja wa Mikoa na Watendaji wengine linalofanyika katika hoteli ya Naura Springs, Arusha. Kongamano linakusudia kuwajengea uwezo wa kiuongozi wa kusimamia uuzaji wa nyumba zinazojengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini. Katika kongamano hilo, mada mbalimbali zinaendelea kutolewa ikiwemo kuwajali wateja, misingi ya uhusiano na ujenzi wa taswira ya Shirika na uwekezaji katika sekta ya usimamizi na uendelezaji wa Miliki.

Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba (NHC), David Shambwe akitoa mada kwenye kongamano hilo. Shambwe alizungumzia hatua muhimu za kuibua miradi kuitekeleza na hatimaye kuiuza kwa ufanisi kwa wateja na kufuatilia malipo baada ya kuuza nyumba zinazojengwa maeneo mbalimbali nchini.

Meneja wa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Tuntufye Mwambusi akizungumza kwenye kongamano hilo.

Mkurugenzi mkuu wa NHC, Nehemia Kyando Mchechu alipata nafasi ya kujadiliana na  mameneja na watumishi wa shirika la Nyumba la Taifa waliohudhuria kongamamo la Arusha kuhusiana na mafanikio na changamoto zinazowakabili.

Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa Felix Maagi na Haikamen Mlekio wakifuatilia mada na mijadala inayoendelea katika kongamano hilo.

Bofya hapa kwa picha zaidi.

No comments:

Post a Comment