Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 8 January 2015

BANK M KUBORESHA ZAIDI HUDUMA KWA WATEJA WAKE

Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Bank M, Allan Msalilwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Hayatt Regency, jijini Dar es Salaam juu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Bank M, Jacqueline Woiso akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu uboreshaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo.

Bank M imesema imeendelea kuboresha huduma kwa wateja katika uendelezaji wa viwanda pamoja na mikopo katika miradi ya jamii ikiwepo kudhamini maji.

Akizungumza na waandishi jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Hayatt Regency Jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Biashara wa Benki M, Jacqueline Woiso, alisema kufanya hivyo ni kutaka wateja wa Bank M kuendelea kunufaika.

Alisema mikopo waliositisha ni ya nyumba pamoja na elimu na kufungua milango ya mikopo kwa taasisi kwa ajili ya maji na viwanda ili kuwezesha wananchi kunufaika katika viwanda pamoja na maji.

Woiso alisema Bank M inawakaribisha wateja wapya kujiunga na benki hiyo ili kuweza kunufaika na huduma mpya zitakazoweza kusaidia jamii kupata maendeleleo.

Aidha alisema huduma nyingine ni uwekaji wa mashine ya kukusanyia fedha kutoka kwa wateja ili kuondoa usumbufu kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Chalila Kibuda, Globu ya Jamii, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment