Meneja chapa wa Serengeti Premium Lager, Bw. Rugambo Rodney akibonyeza kitufe wakati wa kuchezesha droo ya nne kutafuta mshindi wa tatu wa Limo Bajaj katilka shindano la Tutoke na Serengeti ambapo Isaack Edward Amaro ameibuka mshindi. Katikati ni msimamizi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Mrisho Milao na kulia ni mhasibu wa kampuni ya Serengeti (SBL) Monica Labre. Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Meneja chapa Serengeti Premium Lager, Rodney Rugambo akiongea na mshindi wakati wa kuchezesha droo ya nne kutafuta mshindi wa tatu wa Limo Bajaj katilka shindano la Tutoke na Serengeti. Kulia ni msimamizi kutoka michezo ya kubahatisha, Mrisho Milao.
Akiongea kwa njia ya simu, Bw. Isaack
alisema “Shukrani za dhati kwa kampuni ya SBL nilikuwa naelekea kukata tamaa
katika mashindano haya nikiamini kwamba bahati haikuwa upande wangu. Nilikuwa
na matumaini kidogo sana ya kushinda”.
Meneja chapa Serengeti Premium Lager, Rodney Rugambo akiongea na mshindi wakati wa kuchezesha droo ya nne kutafuta mshindi wa tatu wa Limo Bajaj katilka shindano la Tutoke na Serengeti. Kulia ni msimamizi kutoka michezo ya kubahatisha, Mrisho Milao.
Droo ya nne ya Tutoke na Serengeti imefanyika jana katika makao makuu ya kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL)
yaliyoko Chang’ombe, ambapo Bw. Isaack Edward Amaro mwenye umri wa miaka 25 na
mkazi wa Rombo ameibuka mshindi wa tatu wa Limo Bajaj.
Bw. Isaack Edward amepokea habari
njema za ushindi wa Limo Bajaj akiwa safarini kuelekea kijijini kusherehekea
sikukuu za mwisho wa mwaka.
“Serengeti Breweries
itamkabidhi Bw. Isaack Limo Bajaj wiki ijayo. Bajaji hii imelipiwa kila kitu,
gharama za usajili na usafirishaji itakuwa ni jukumu la SBL na si mshindi. “Isaack
hataingia gharama yoyote”..alisema Meneja Chapa wa Bia ya Serengeti Premium
Lager, Bwana Rugambo Rodney wakati akiongea na waandishi wa habari
waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.
Sambamba na hilo Bw. Ombeni
William Mushi ambaye ni mwalimu “Moshi Secondary school” ameibuka mshindi wa wiki
wa fedha taslim Tsh. 100,000.
Ujumbe kutoka kwa afisa wa B-Pesa
ulithibitisha kwamba droo hii ya nne ilikuwa na washiriki wengi na wateja
wamekuwa wakivutiwa na kupelekea idadi ya washiriki kuongezeka.
Rodney aliendelea kuwakumbusha wateja kwamba
ili kushiriki katika kampeni hii wanatakiwa kuwa na umri usiopungua miaka 18 na wanatakiwa kununua bia ya Serengeti Premium Lager na
kuangalia chini ya kizibo ambako watakuta namba ambazo zinatakiwa kutumwa kwa SMS
kwenda namba 15317 na watapata nafasi ya kuingia kwenye droo na kuweza kujishindia
zawadi mbalimbali kama vile:- Limo Bajaj, safari ya wawili kwenda katika mbuga
za wanyama, fedha taslim shilingi 100,000/=, vilevile mteja anaweza kujishindia bia
za bure ambazo zinapatikana katika baa zote hapa nchini pamoja na punguzo la shilingi 300/=katika bia
za Serengeti premium Lager. Kadiri unavyoshoriki kutuma
namba ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya kushinda.
Kwa maelezo zaidi tembelea :-
Kurasa za
Serengeti premium Lager Face book/Twitter na YouTube kwa video.
KUHUSU SERENGETI BREWERIES LIMITED
Serengeti
Breweries Limited inajihusisha na utengenezaji, uandaaji, uuzaji na usambazaji
wa vinywaji vya kimea na shayiri na uwele hapa Tanzania.
Ikiwa na makao makuu yake
hapa Dar es Salaam, bidhaa za Serengeti ni pamoja na:- Serengeti Premium Lager,
Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager,
Pilsner Lager, Senator, The Kick na Guinness®..
No comments:
Post a Comment