Mkurugenzi Mkuu wa B-Pesa, Bw. Sean Merali, (kushoto) Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleimani Kova (wa pili kushoto), na Mkurugenzi wa Benki ya I&M, Michael Shirima (wa tatu toka kushoto), na Shameer Patel, Meneja Mkuu wa Benki ya I&M (wa pili kulia) wakikata keki kama ishara ya uzinduzi wa ushirikiano mpya kati ya B-Pesa na Benki ya I&M, ambapo ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa kuwafikia wateja wao kiurahisi kwa taasisi hizo. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikua ni Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki katika uzinduzi wa ushirikiano wa B-Pesa na Benki ya I&M, wakimsikiliza mgeni rasmi Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova (hayupo pichani), wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa B-Pesa na Benki ya I&M, Kamanda kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, (wa kwanza kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa B-Pesa, Sean Merali, (wa kwanza kushoto). Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wa B-Pesa na Benki ya I&M, Kamanda kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya I&M Michael Shirima (wa tatu toka kushoto) wakivuta pazia kama ishara ya kuzindua rasmi ushirikiano mpya wa taasisi za B-Pesa na Benki ya I&M. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa B-Pesa, Sean Merali (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki ya I&M, Michael Shirima, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa taasisi hizo mbili, katika hafla iliyofanyika ndani ya hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana.
Dar es Salaam 17 Desemba, 2014. B-PESA jana imetangaza ushirikiano mpya kati yake na benki ya I&M kwa kuzindua kadi mpya ya B-PESA EMV pamoja na PIN card ikiwa na lengo la kusambaza huduma kwa wateja wake na kwa Watanzania kwa ujumla.
Wateja wa B-PESA wanaweza kuweka au kuchukua fedha zao kupitia matawi yoyote ya benki ya I&M ambayo yanapatikana nchi nzima.
B-PESA inatoa fursa kwa wateja wake kupitia njia mbalimbali za kielectroniki kama vile web portal au njia ya vifaa vya simu kwa njia ya programu za Android na USSD kutumia kadi zao B-PESA. Kadi za B-PESA zinaweza kujazwa katika maduka yote ya EzyPesa baada ya makubaliano na Zantel ambayo yalifanywa mwanzoni mwa wiki hii.
B-PESA ni kampuni ya kwanza na ya kipekee kuanzisha huduma ya haraka kwa wafanya biashara wakati huo huo ikiboresha huduma ya kadi. B-PESA pia ina mfumo wa lugha mbalimbali kwa masaa 24 kwa siku 7 katika vituo mbalimbali vya huduma nchini Tanzania kwa ajili ya maajenti wanaotumia lugha za Kiswahili, Kingereza na Kihindi
B-PESA imefanikiwa kuleta mabadiliko katika secta ya huduma ya kifedha kwa kuleta urahisi kwa watu walio au wasio na akaunti za benki kufanya miamala au kufanya malipo mbalimbali pasi na kuwa na fedha taslim mkononi. Hii ni njia salama na rahisi Zaidi kwa mtu kubeba na kutumia pesa ambapo B-PESA hutoza kiwango cha chini cha huduma ya muamala.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, katika hoteli ya Serena Jijini Dares salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa B-PESA, Bwana Sean Merali alisema kwamba uhusiano kama huu ni muhimu kwa benki nyingine za Afrika Mashariki katika soko hili ambalo limekuwa likibadirika hasa ukizingatia kwamba uhitaji wa huduma bora na za teknolojia mpya zimekuwa zikihitajika sana na wateja wetu’.
Bwana Merali aliongeza kwamba wako katika hatua za mwisho kuzindua huduma ya kadi za B-PESA na benki ya Stanbic Bank pamoja na benki ya DTB, zote zikiwa zimepata uthibitisho kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
B-PESA imejipanga pia kupeleka huduma hii katika nchi nyingine za Afrika Mashariki ifikapo 2015, ikianzia na Kenya na Uganda ambazo tayari zimeshaweka miundombinu kwa ajili ya huduma hiyo.
Benki ya I&M kwa sasa ina matawi sita nchini Tanzania, vituo muhimu vikiwa Dar es Salaam, Moshi, Arusha na Mwanza. Kwa mtandao huu, kwa pamoja inaongeza urahisi Benki ya I&M na kwa wateja wa B-PESA. Wateja watapata fursa pia ya kufurahia huduma nyingine nyingi kutoka kwa B-PESA ikiwa ni pamoja na zaidi ya mawakala 2,500 ambao wanapokea kadi za B-PESA.
B-PESA pia imezawadia wateja wake katika kipindi hiki cha sherehe za mwisho wa mwaka ambapo mmiliki wa kadi atapata punguzo la asilimia 50 ya bidhaa atakazonunua kwa kutumia kadi ndani ya siku 12.
No comments:
Post a Comment