Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 25 September 2014

BENKI YA NMB YAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI WILAYANI NGORONGORO

Meneja wa kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishubo akimkabidhi msaada wa madawati Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Papakiny Kaai kwa ajili ya shule za msingi za Loliondo. Kulia ni Meneja wa Huduma kwa wateja katika tawi la NMB Loliondo Bw. Abraham Mbise.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Papakiny Kaai akitoa neno la shukhrani kwa uongozi wa NMB baada ya kupokea msaada wa madawati sabini kwaajili ya shule za msingi zilizopo Loliondo.

Benki ya NMB imetoa msaada wa madawati 70 kwaajili ya kusaidia shule za msingi zilizopo wilayani Ngorongoro. Thamani madawati hayo ni shilingi milioni 5. 

Msaada huo unalengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji kwa wanafunzi wa shule za msingi za wilayani Ngorongoro.
Huo ni mwendelezo wa Benki katika kuchangia huduma za kijamii kwa njia ya kurudisha sehemu ya faida inayopatikana kwa wananchi na kuifanya benki ya NMB kuwa karibu zaidi na watanzania.



Meneja wa NMB kanda ya Kaskazini Bi. Vicky Bishubo alisema msaada huo ni mwitikio wa NMB kusaidiana na wananchi pamoja na serikali katika kutatua changamoto za uhaba wa madawati kwa wanafunzi wa wilaya ya Ngorongoro.


Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw. Papakiny Kaai aliishukuru benki ya NMB kwa kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto mbalimbali zilizomo kwenye wilaya ya Ngorongoro na taifa kwa ujumla hasa katika elimu na afya.

No comments:

Post a Comment